TANGAZO


Sunday, March 1, 2015

Washindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon watunukiwa zawadi zao

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga, (kulia) akimkabidhi mshindi wa kwanza katika mbio za walemavu wanawake Linda Macha zawadi ya kiti cha walemavu kutoka kwa wadhamini wa mbio hizo Gapco leo mjini Moshi kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa wa mbio za Tigo Kili Half Marathon wanawake Grace Kimanzi zawadi ya shilingi milioni mbili kutoka kwa Tigo wadhamini wa mbio hizo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa wa mbio za Tigo Kili Half Marathon wanaume Ismail Juma kutoka Babati zawadi ya shilingi milioni mbili kutoka kwa Tigo wadhamini wa mbio hizo. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mathias Chikawe akimkabidhi zawadi David Ruto mshindi wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon (Km 42.2) zawadi ya shilingi milioni nne kutoka kwa wadhamini wakuu wa Kilimanjaro Marathon bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Kushoto ni James Bokella, Meneja Mauzo na Usambazaji TBL Kanda ya Kusini.
Mshindi wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon (42.2km), David Ruto akimaliza mbio za Kilimanjaro Marathon leo, mjini Moshi ambapo alitetea ubingwa wake. Ruto ndiye mshindi wa mbio hiyo mwaka jana pia. 
Mshindi wa Tigo Kili Half Marathon wanaume (21.1km), Ismail Juma akimaliza mbio za Kilimanjaro Marathon jana mjini Moshi. 
Mshindi wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon wanawake (42.2km), Fabiola William akimaliza mbio za Kilimanjaro Marathon leo mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment