Serikali ya Nigeria imekiri kwamba raia,wakiwemo watoto wametekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram katika majuma ya hivi karibuni.
Msemaji Mike Omeri amesema kuwa ni vigumu kukisia idadi ya watu ambao wametekwa wakati wapiganaji wa Boko Haram wakitoroka wakati wa mashambulizi dhidi yao yanayotekelezwa na vikosi vya kijeshi kutoka Nigeria,Chad na Niger.
Lakini msemaji wa Nigeria alipinga madai kwamba zaidi ya watoto 500 walikuwa hawajulikani waliko kutoka mji uliochukuliwa na jeshi Damasuk karibu na mpaka wa Niger.
Nigeria imetangaza kwamba inafunga mpaka wake kuanzia siku ya jumatano usiku hadi jumapili huku uchaguzi wa urais ukifanywa.
No comments:
Post a Comment