Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz akizungumza na washiriki wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), akifurahia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakionyeshwa na vijana wakati wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz na wapili kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
Wanafunzi kutoka
shule za Feza wakiburudisha wakati wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni
lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa
Mwalimu Nyerere jana jijini Dar es Salaam na kuhusisha washiriki kutoka nchi 19
wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya lugha ya kiswahili. (Picha zote na Genofeva Matemu -
Maelezo)
Na
Lorietha Laurence na May-Zuhura Simba -Maelezo
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ameeleza kuwa lugha ina
mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwa itakuzwa sambamba na maendelao
ya teknolojia.
Kauli hiyo ameitoa jana
jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni na
kufafanua kuwa tamasha hilo limeonyesha
kukua kwa lugha ya Kiswahili ambao ni utambulisho wa nchi yetu tangu kupatikana
kwa uhuru.
“Mkusanyiko wa leo umeanzisha safari ndefu ya
kukuza lugha yetu ya Taifa toka ngazi za chini hadi za kimataifa, hivyo
Tanzania imefarijika kuwa mwenyeji wa shughuli hii muhimu “alisema Mhe. Dkt. Mukangara.
Aliongeza kuwa kwa
upande wa serikali ya Tanzania imechukua
hatua mbalimbali ya kukiendeleza Kiswahili kwa kukifanya kuwa lugha ya kufundishia kuanzi shule ya Msingi hadi
Elimu ya Juu.
Dkt. Mukangara ametoa
wito kwa vijana kujifunza Kiswahili na kuitumia lugha hiyo kuweza kujipatia
ajira kwa kutangaza utumiaji wa bidhaa
za lugha na utamaduni ambazo zina thamani kubwa kiuchumi.
“Lugha ni sawa na kiwanda ikitumiwa vizuri
italeta ajira kwa jamii husika na kutumika kama lugha ya kufundisha wageni mbalimbali wanaokuja nchini na hata
nchi za nje kwa kuipa hadhi ya kuzungumzwa sehemu mbalimbali” alisema Mhe. Dkt.
Mukangara.
Kwa Upande wa muandaaji
wa tamasha hilo ambaye ni Rais wa Asasi za Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw.
Ali Akkiz amesema kuwa kupitia tamasha
hilo wameweza kutangaza vivutio mbalimbali vya kiutamaduni vya jijini Dar es salaam na Zanzibar.
“Kwa kweli watoto
wamefurahi kushiriki katika tamasha hili kwa kuweza kutembelea sehemu zenye
vivutio vya utamaduni pamoja na historia najua wataondoka na taswira nzuri ya
kutokuisahau nchi ya Tanzania” alisema Bw. Akkiz
No comments:
Post a Comment