Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan akikabidhi kiti maalum cha kujisaidia pamoja na kiti cha magurudumu kwa mama huyo mlemavu.
MBUNGEwa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan (CCM) ametoa msaada wa kiti cha magurudumu kwa Rehema Nditi mkazi wa Magomeni Mwembe Chai kama msaada kutokana na taabu aliyokuwa akiipata.
Idd Azzan ametoa msaada … ambapo baada ya kuona Rehema Nditi kupataa tabu ya kukosa kiti hicho.
Mbunge huyo amekua akisaidia maendeleo mbalimbali ikiwemo shughuli za kijamii ndani ya jimbo lake hilo.
Aidha, Mh. Iddi Azzan ametoa rai kwa Watanzania kuungana nae katika kuchangia pesa kwa ajili ya kununua Bajaji ambayo itafanya biashara ili waweze kuendesha maisha ya kila siku.
“Watanzania tuungane kumchangia mama huyu kiasi chochote ilikununua bajaji kwa ajili ya kufanya biashara ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku kupitia kipato cha biashara hiyo ya Bajaji” alieleza Idd Azzan.
Kwa upande wake, Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania, Kinachoerushwa na kituo cha Channel Ten, Hoyce Temu amefungua michango hiyo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 500,000/- ili kuhamasisha na wengine kuchangia.
Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwenye ofisi za Mbunge wa jimbo la Kinondoni ama unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Rehema Nditi kupitia namba TIGO PESA +255 719-543075 AU M-PESA +255 754 097 527
No comments:
Post a Comment