Mapigano makali yanashuhudiwa nje na ndani ya uwanja wa ndege katika mji wa Aden nchini Yemen.
Taarifa zinasema maafisa wa polisi waaminifu kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Ali Abdullah Saleh, walishambulia sehemu moja ya uwanja wa ndege, lakini wakakabiliwa na makundi ya usalama yanayomuunga mkono rais wa sasa, Abed Rabbo Mansour Hadi.
Milipuko kadhaa imetokea katika uwanja huo na abiria waliagizwa kushuka kwenye ndege iliyokuwa inatarajiwa kuondoka kuelekea Cairo.
Washambuliaji watatu waliuwawa katika mapigano huku kumu kati yao wakitiwa mbaroni.
Aden ni ngome kuu ya rais Abdrabbuh Mansour Hadi, aliyekwepa nyumbani alikokuwa anazuiliwa katika mji mkuu Sanaa baada ya waasi wa madhehebu ya kishia - Houthi kulidhibiti kikamilifu eneo hilo mnamo mwezi Januari.
No comments:
Post a Comment