Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiambatana na wenyeji wake baada ya kuwasili mjini Musoma.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Mara Adam Ngalawa baada ya kuwasili mjini Musoma.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza wimbo wa Tanzania uliokuwa unaimbwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisangula.
Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala, akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati), ramani ya Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma. Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal kuzungumza na wananchi kwenye eneo la mradi
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akizungumza na wananchi.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu Aseri Msangi na kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Maghembe.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati) akikata utepe wa Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto kwake ni Balozi wa Ufaransa nchini, Melika Berak na viongozi wengine wa chama.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak.
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Nadhifa Kemikimba akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia mifupa.
Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Maji Kitaifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba akizungumza na wananchi juu ya maadhimisho.
Makamu
wa Rais, Dkt. Bilal akimpa kikombe Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na
Uhandisi wa Umwagiliaji wa Chuo cha Maji, Eng. Pantaleo Tumbo ikiwa ni moja ya
zawadi zilizotolewa kwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Maji.
Na Hussein Makame-MAELEZO, Musoma
MAKAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohgamed Ghalib Bilal amesema kuwa kila ahadi ya Serikali
iliyotolewa itatimizwa ili kuhakikisha kuwa inaacha kazi nyepesi kwa viongozi
watakaokuja katika kuendeleza maendeleo ya Tanzania.
Dkt. Bilal aliyasema hayo kwenye kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mara
yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Mandeleo Endelevu.
Katika kilele cha Maadhimisho hayo, Dkt. Bilal aliweka
jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira Mjini Musoma ambao utagharimu Shilingi Bilioni 44 hadi
kukamilika kwake.
“Tumewaahidi kupata maji na hilo tutatekeleza.Kila
ahadi ya Serikali itatimizwa swali ni muda na wakati lakini kwa kweli
hatukusudii kuwaacha njiani, mambo tuliyosema tutayafanya ili tuwaachie
watakaokuja kazi nyepesi ya kuendeleza maendeleo ya nchi yetu” alisema Dkt.
Bilal.
Mradi huo mkubwa wa maji unatarajiwa kukamilika mwezi
Aprili, 2015 ambapo Dkt. Bilal alisema mradi huo utakapokamilika itaipatia Manispaa ya Musoma maji ya uhakika kwa
asilimia 100.
Aliongeza kuwa mafanikio ya mradi huo pia ni kuongezeka
kwa uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 10,000 za sasa kwa siku, hadi mita
za ujazo 36,000 kwa siku.
Dkt. Bilal alitoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya
Musoma na mkoa wa Mara kutunza mradi huo na miradi yote inayoendelea
kutekelezwa ili iendelee kuwasaidia wananchi na vizazi
vijavyo.
“Na juu ya haya yote, ni msisitizo
katika utunzaji endelevu wa mazingira yetu ili yaendelee kutuhifadhi. Aidha,
teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa ni maeneo ambayo
yatatuhakikishia kwamba tunakuwa na huduma endelevu ya rasilimali ya maji”
alisema.
Alisema Tanzania haina budi kuwa na mikakati ya
makusudi kukabiliana na changamoto hizo, jambo ambalo Serikali imeanza
kulifanyia kazi.
Alifafanua kuwa uhaba wa maji na
kutopatikana kwake kwa uhakika kunaleta athari mbaya katika shughuli zote za
kiuchumi.
“Majanga yanayohusiana na maji kama vile, mafuriko na
ukame kwa kiwango kikubwa ni maafa yanayojitokeza mara nyingi katika sehemu
mbalimbali duniani hivi sasa” alisema Dkt. Bilal na kupngeza kuwa:
“Vifo, uharibifu wa mali, makazi na miundombinu vina
athari kubwa kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kikundi, jamii na hata Taifa”.
Hivyo, alitoa wito kwa wadau wote kuunganisha nguvu
pamoja katika kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kwani,
mabadiliko hayo yana athari kuanzia kwenye kupungua kwa misitu na vyanzo vya
maji.
Alitaja athari nyingine kuwa ni kupungua kwa
rasilimali za maji juu na chini ya ardhi; kuathirika kwa ubora wa maji ya
kunywa; hadi kukua kwa utoaji wa gesi ya ukaa.
Hata hivyo alisema, Serikali ya
Tanzania itaendeleza juhudi za kuhakikisha inawafikishia wananchi maji safi na
salama katika maeneo ya nchi ambayo yamekosa huduma hiyo.
Aliwakumbusha wananchi kuwa wana jukumu
kubwa la kutunza vyanzo vya maji popote pale vinapopatikana na kwamba wana kubwa
kwenu wananchi ni kutoa mchango unaostahili katika usimamizi na uendelezaji wa
rasilimali za maji.
Akimkaribisha
Dkt. Bilal, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema wizara yake
itajitahidi na kufanya kila linalowezekana ili katika kipindi kisichozidi miezi
mitatu maji yatoke mjini Musoma na wananchi wafurahie huduma hiyo.
Alisema
katika kipindi cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, viongozi mbalimbali walishiriki
katika kukagua miradi ya maji na kutembelea wilaya zote za Mara na kuweka mawe
ya msingi na kuzindua miradi ya maji ambayo imekamilika.
No comments:
Post a Comment