Jeshi la Nigeria limesema limeurejesha mji wa Bama uliko kaskazini mashariki mwa Nigeria kutoka kwa wapiganaji wa Kiislam wa kundi la Boko Haram.
Wapiganaji wa Boko Haram walikuwa wakiudhibiti mji wa Bama, ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno tangu mwezi Septemba mwaka jana.
Mike Omeri, msemaji wa Rais Goodluck Jonathan, amethibitisha kuwa majeshi ya Nigeria yaliingia Bama.
Alipoulizwa na BBC ni kwa nini imechukua wiki mbili kuutwaa tena mji huo kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge, amesema jeshi lilikosa zana muhimu.
No comments:
Post a Comment