Kundi la Islamic State linasema kuwa wapiganaji wake waliendesha mashambulizi ya kujitoa mhanga kwenye misikiti miwili nchini Yemen ambapo zaidi ya watu 130 waliuawa.
Washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walilenga waumini kwenye mji mkuu Sanaa wakati wa maombi ya Ijumaa.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na waumini wanaowaunga mkono waasi wa Shia wanaofahamika kama Houthi ambao walichukua udhibiti wa mji wa Sanaa mwaka uliopita.
Zaidi ya watu 200 walijeruhiwa wakati wa mashabulizi hayo ambapo wito wa kuwaomba watu kutoa damu umekuwa ukitolewa.
No comments:
Post a Comment