Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane ameitwa kwa mara ya kwanza kuichezea Timu ya Taifa ya England.
Kane, mwenye Miaka 21 ambae amefunga Bao 26 kwa Mechi 42 Msimu huu, ni mmoja wa Wachezaji 24 waliotangazwa na Kocha Roy Hodgson leo.
Akitangaza Kikosi hicho, Hodgson alisema: "Nchi nzima inavutiwa na Harry Kane. Ingeshangaza kama tusingemchagua!"
Kikiso hicho cha England kitacheza na Lithuania Uwanjani Wembley, London hapo Machi 27, kisha kwenda Turin kucheza na Italy Mechi ya Kirafiki hapo Machi 31.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City)
Mabeki:Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Southampton), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Luke Shaw (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United), Kyle Walker (Tottenham Hotspur).
Viungo: Ross Barkley (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Manchester City), Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Theo Walcott (Arsenal).
WashambuliajiI: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Arsenal).
No comments:
Post a Comment