Serikali yahitaji (Laboratory
Technician) 10,000
Na Anitha Jonas – MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imesema inauhitaji wamafundi
sanifu 10,000 wa maabara (Laboratory Technicians) mpya zionazojengwa
nchini.
Hayo yameyasema na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bungeni
Mjini Dodoma, Mhe.Hawa Ghasia alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chwaka, Yahya
Kassim Issa (CUF).
Katika swali lake Issa alitaka kujua kwa nini Serikali huwapa mikataba watumishi waliostaafu wakati wapo vijana wengi ambao hawana kazi.
Waziri Ghasia alisema Serikali hutoa
mikataba kwa baadhi ya kada ambazo bado hazijitoshelezi kutokana na kuwa na wataalamu wachache.
“Kwa mfano kwa sasa Serikali ina mahitaji makubwa wa mafundi sanifu wa maabara kwa ajili ya kusimamia maabara zetu zinazojengwa walipo kwa sasa hawafiki 1,000 wakati mahitaji ni 10,0000,” alisema Ghasia.
Awali akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo, Ghasia alisema sio sera ya Serikali kuwaajiri wastaafu isipokuwa pale tu inapoonekana ni kwa manufaa ya umma kutokana na mahitaji makubwa katika sekta husika.
Alisema vijana na wasomi waliohitimu
vyuo mbalimbali hapa nchini hupatiwa ajira kulingana na mahitaji ya bajeti iliyopo.
Waziri Ghasia alisema Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Pensheni
kwa Watumishi wa Umma sura namba 371, mtumishi wa umma anayo hiari ya kustaafu kwa hiyari akifikisha umri wa miaka 55.
aibu Waziri wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo
Mhe.Juma Nkamia akijibu swali la msingi
la Mhe.Abdallah Ali (Mb) wa Kiwani tarehe 20.03.2015,Mjini Dodoma.
Serikali kuboresha kiwango cha Soka nchini
Na Anitha
Jonas – MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yajipanga kufanya Utafiti wa
kushuka kwa kiwango cha soka nchini hayo yasemwa Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni
na Michezo Mhe.Juma Nkamia,Bungeni Mjini Dodoma tarehe 20.03.2015.
Mhe.Nkamia aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali la
Mhe.Abdallah Ali Mbunge wa (Kiwani)lililohoji juu ya kushuka kwa kiwango cha
soka nchini ikilinganishwa na miaka ya 1970 na 1980,na kusema kushuka kwa soka
nchini kunategemeana na vigezo mbalimbali ikiwemo ligi za ndani,Idadi ya Timu
zinazoshiriki pamoja na matokeo ya Kimataifa na Viwango vya FIFA.
“Serikali inatoa pongeza Shirika la NSSF pamoja na Timu ya Real Madrid kwa kuanzisha mfumo
mzuri wa kuinua soka la Tanzania kwa kuanzisha timu za kuibua vvijana wenye
vipaji vya kucheza soka nchini”,alisema Mhe.Nkamia.
Katika kipindi cha maswali ya nyongeza Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Ilala, ambaye ni mdau mkubwa wa
michezo alihoji juu ya mpango wa Serikali wa kuweka picha za wachezaji maarufu
wa zamani katika Uwanja wa Taifa mfano kama mchezaji Abdallah Kibadeni na wengine waliyoiletea sifa
kubwa taifa.
Naye Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo alijibu
kuwa serikali inashughulikia suala hilo ila kumekuwa na tatizo kubwa la
upatikanaji wa picha za wachezaji hao wazamani lakini Wizara itajitahidi kulighulikia
hilo kwa ushirikiano na Idara ya Habari Maelezo.
Mbali na hayo Mhe.Nkamia alisema kigezo cha wachezaji wa miaka ya 1970 hadi 1980 kulikuwa na idadi ndogo ya
wachezaji ukilinganisha na sasa pia idadi ya klabu za soka zilikuwa hazidi hata
30 kwa wakati huo bali kwa sasa kuna
zaidi ya vilabu 100.
Pia katika miaka ya 1980 Tanzania ilikuwa na wachezaji wasiozidi
watano waliokuwa wakicheza soka la kulipwa na kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa
kuna wachezaji zaidi ya 15 wanaocheza soka la kulipwa kwa wakati mbalimbali nje
ya nchi.
Serikali ya Pinga Hoja ya Kuanzishwa kwa Mwenge Mikoani
Na Anitha Jonas- MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imepinga Suala la kuanzishwa kwa Mwenge utakao kuwa
unakimbizwa kwa kila Mkoa kwa dhana ya kujaribu kupunguza gharama za Mbio za Mwenge
nchini,hayo aliyasema Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
Mhe.Juma Nkamia alipokuwa akijibu swali Bungeni Mjini Dodoma.
Mheshimiwa Nkamia alisema kuwa kuanzishwaji kwa Mwenge kwa
kila Mkoa kutaondoa dhana halisi ya kuwepo
kwa Mwenge nchini kwani falsafa ya Mwenge ni Mshikamano kwa Taifa,Umoja kwa
Taifa,Amani kwa Taifa pamoja na Maendeleo kwa Taifa.
“Suala la kuwepo na
Mwenge mmoja Kitaifa ni kitu sahihi kabisa na hata tukiangalia nchi za wenzetu
mfano Jumuiya ya Madola wanakifimbo cha malkia ambacho huzungushwa katika nchi
zote za Jumuiya ya Madola,pia upo Mwenge wa Olimpiki ambao huzungushwa dunia
nzima hivyo si busara kwa nchi yetu kuanzisha utaratibu wa Mwenge kwa kila Mikoa”,alisema Nkamia.
Hoja hiyo ya kupunguza gharama za mwenge pamoja na suala la
kuanzishwa kwa Mwenge katika mikoa ni
swali lilihojiwa na Mhe.Meshark Opulukwa
Mbunge wa Meatu katika kipindi cha maswali na majibu na huku akiishauri
serikali kutengeneza Mwenge huo hata kwa mabati chakavu kupunguza gharama.
Akijibu swali hilo Mhe. Nkamia alisema kutengeneza Mwenge kwa
Mabati chakavu ni kuudhalilisha Mwenge na kuonyesha kutodhamini na kuelewa
umuhimu wa Mwenge kwa Taifa.
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wakiwa wamesimama ndani ya Bunge
mara baada ya kutambulishwa kwa uwepo wao, Mjini Dodoma tarehe 20.03.2015.
Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Umiliki Silaha wasomwa kwa mara ya Pili Bungeni
Na Anitha Jonas – MAELEZO, Dodoma.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Pereira Silima amesoma Muswada wa Sheria ya Kupendekeza kutungwa kwa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha ya mwaka 2014 Bungeni Dodoma kwa mara ya pili tarehe 19 Machi 2015.
Mhe.Silima alisema Serikali imeona umuhimu wa kutunga Sheria hii ya Udhibiti wa Umiliki wa silaha kutokana na kukabiliana na tatizo la kuwepo na watu wengi wanao kumiliki silaha kinyume na sheria pamoja na kufanya matumizi mabaya ya silaha.
“Serikali imekubaliana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na mfumo wa kisheria baada ya kusaini na kuridhia maazimio ya kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu na sheria hii inaelekeza wazi kuwa mtu anaweza kumiliki silaha akiwa na umri wa kuanzia miaka 25,”alisema Mhe.Silima.
Mhe.Silima aliendelea kusema kuanzia mwaka 2000 mpaka 2013 serikali ilikamata zaidi ya silaha 34,156 zilizokamatwa katika operesheni mbalimbali na silaha hizo ziliteketezwa.
Kwa upande wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mhe.John Chiligati aliipongeza serikali kupitia kifungu chake cha 19 kinachoeleza kuwa sihala zote zitawekwa alama ya utambuzi wa kitaifa,Pia baada ya sheria hii kupitishwa suala hilo lizingatiwe.
“Kamati inapenda kuishauri Serikali katika kifungu cha 20(2) kuondoa adhabu ya kulipa faini kwa mtu anayemiliki silaha kinyume na sheria na badala yake ni kutumikia kifungu kisichozidi miaka mitano”,alisema Mhe.Chiligati.
Mhe.Chiligati aliendelea kusema kamati imeridhia marekebisho ya Serikali ya kuongeza idadi ya wajumbe wa kamati ili iwe na uwakilishi mpana kutoka sekta binafsi,Pia Kamati imeshauri kifungu cha 5(3) kisomeke kuwa mtu yeyote atakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati endapo ni raia wa Jamhuri ya Muungano.
Naye Mbunge wa Nkasi Kusini Mhe.Desderius Mipata ameipongeza Serikali kwa kuunda Sheria itakayo dhibiti umiliki wa silaha nchini, pia ameishauri serikali kuangalia ni namna gani itadhibiti maduka yanayouza silaha nchini.
No comments:
Post a Comment