Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Anne Kilango akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Roseweeter Kasilika (Viti Maalum) lilihoji juu ya Serikali kutilia maanani Mwongozo kwa Elimu ya Awali,Mjini Dodoma tarehe 24/03/2015.
Waziri Mkuu Mhe. Peter Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Amos Makalla ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati kikao cha bunge kinaendelea Mjini Dodoma, tarehe 24/03/2015.
Mbunge wa Jimbo la
Ole (CUF)Mhe.Rajab Mbarouk
akichangia hoja katika Muswada wa
Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Madawa ya Kulevya, Mjini Dodoma tarehe
24/03/2015.
Na Anitha
Jonas-MAELEZO,Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe.Jenista Mhagama amesoma Muswada wa
Sheria ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya wa mwaka 2014 kwa mara pili Bungeni
Mjini Dodoma tarehe 24.03.2015.
Mhe.Mhagama alisema kupitia Muswada
huu Serikali itaunda chombo kitakachosimamia na kudhibiti biashara ya
Madawa ya Kulevya pamoja na kuanzisha vituo vitakavyo toa tiba kwa waadhirika
wa madawa ya kulevya.
“Sehemu ya sita ya Muswada
huu unahusu uanzishwaji wa Mfuko wa Udhibiti wa Kupambana na madawa ya kulevya
na na pia sehemu tano inahusu kufilisi mali wafanyabiashara za madawa ya
kulevya pale wanapitiwa hatiani,hivyo basi sheria hii itaipa meno Mamlaka itakayoundwa
kwa ajili ya kupambana nawafanya biashara wa Madawa ya Kulevya pamoja na wahusika wote wanajihusisha na madawa ya kulevya,ikiwa ni
pamoja na ujazaji wa fomu kwa watuhumiwa watakao kamatwa katika biashara
hizo,”alisema Mhe.Mhagama.
Kwa upande wa maoni ya kambi
ya Upinzani inayoshughulikia masuala ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na
Bunge) yaliyosomwa na Mhe. Rajab Mbarouk
alisema kambi ya Upinzani inaishauri Serikali kwa ujumla katika vifungu
vyake mbalimbali vinavotoa adhabu ya faini viondolewa na badala yake iwe ni
kifungo cha maisha au kunyongwa mpaka kufa.
Kwa upande wa uchangia wa
maoni kutoka kwa wabunge juu ya muswada huo Mhe.Mwibara Lugola (Mb) CCM
aliishauri Serikali kutoa hukumu kwa watakao kamatwa na madawa papo kwa papo kwa
mfano mtu alinayekamatwa na madawa ya kulevya akiwa ameyameza au kuyabeba.
Pia
alisisiitiza kwa kuiomba Serikali iondoe suala la faini na badala yake iwe ni
kifungo cha maisha au kunyongwa mpaka kufa.
Aidha, naye Mhe. David Silinde (Mb) alitoa maoni kwa Serikali
kwa kuiomba Sheria hii ionyeshe ni namna gani
itadhibiti suala la usafirisha wa madawa ya kulevya katika mipaka yote
ya nchi,vilevile Serikali ifikirie juu kuanzisha mahakama maalum zitakazo
shughulikia kesi za madawa ya kulevya.Pia alipendeza bunge kuwa msimamizi wa
utekelezwaji wa hukumu kwa kesi za madawa ya kulevya na adhabu iwe imetekelezwa
angalau ndani ya wiki mbili.
Katika maoni kutoka kwa wabunge mbalimbali walisema
wanaiomba Serikali kuwa Muswada huu
uangalie ni namna gani utalinda haki ya mtu
kutoa siri ya mtu atakayetoa taarifa za wafanyabiashara wa Madawa ya Kulevya nchini.
No comments:
Post a Comment