Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya akisoma Muswada wa Sheria Mifumo ya Malipo wa Mwaka 2015 katika Mkutano wa 19, Kikao cha Sita Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Amos Makalla akijibu swali kwa lililoulizwa na Mhe. Profesa David Mwakyusa (Mb) wa (Rungwe Magharibi) Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Anne Kilango akijibu
swali liliulizwa na Mhe.Amina Makilagi Mbunge wa Viti Maalum lilohoji juu ya
mchang’anuo wa ada za Vyuo vikuu vya Umma,Bungeni Mjini Dodoma .
.
Na Anitha
Jonas-MAELEZO,Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe.
Saada Mkuya amesoma Muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo nchini wa mwaka 2015 kwa mara ya
pili Bungeni Mjini Dodoma, Sheria hii
imelenga kudhibiti wizi unaofanyika kupitia mitandao pamoja na kuhakikisha serikali
inanufaika kwa kujipatia mapato.
Mhe.Mkuya alisema
chimbuko la Muswada huo ni matokeo ya maboresho yaliyofanywa na Serikali katika
sekta ya fedha nchini yaliyoanza mwaka 1990 na yanayoendelea mpaka sasa pamoja
na maboresho katika sekta ya fedha yaliyosababisha kutungwa kwa sheria ya
mabenki na taasisi za fedha za mwaka 2006 pamoja na sheria ya Benki kuu ya
mwaka 2006.
“Lengo la Muswada huu ni kuboresha Usimamizi,Udhibiti na
Kuimarisha Mifumo ya Malipo nchini,pamoja na kuiweka nchi katika mazingira
mazuri ya ushindani wa kibiashara,halikadhalika kudhibiti changamoto zinazoweza kutokea katika sekta ya fedha na kutengeneza
mazingira bora ya kiufanisi,”alisema Mhe.Mkuya.
Kwa upande wa maoni ya
Kamati ya Upinzani yaliyosomwa na Mhe. Christina Lissu (Viti Maluum -CHADEMA) kwa niaba ya
Mwenyekiti wa kambi ya upinzani ya Wizara ya Fedha Mhe. James Mbatia, Kamati
ilishauri Serikali kuondoa ukomo wa faini na badala yake iwe inasomeka (zaidi ya) kwa ajili ya kumwachia Hakimu kupanga ukomo wa faini
hiyo, hivyo Serikali ifanye mabadiliko katika cha 20 (a) na (b).
Katika kipindi cha uchangiaji
wa maoni Mhe.Musa Azza (Mb) wa Ilala naye
aliishauri serikali kuunda chombo
kitakacho simamia mihamala yote inayofanywa
kupitia mtandao ili serikali iweze kujipatia mapato ambayo yatasaidia
kuendeleza nchi yetu tofauti na sasa fedha nyingi zinapotea na serikali inakosa
mapato.
Naye Mhe.Suzan Lyimo
Mbuge wa Viti Maalum Chadema aliishauri
serikali kuwa sheria hii iangalie suala la mifumo ya mtandao kuwa chini
kwani hili limekuwa liliwagarimu sana wananchi,halikadhalika gharama
zinazotozwa na makampuni ya simu katika Kutoa Pesa na Kuhamisha Pesa kama
Mpesa,Tigopesa na Airtel Money.
Muswada huu na jumla ya
sehemu 12 na Ibara 59 ambazo zimezingatia kuleta manufaa makubwa kwa wananchi
pamoja kuiletea mapato serikali.
No comments:
Post a Comment