Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mikopo hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Urejeshwaji Mikopo, Juma Chagonja na kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi-Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Veneranda Malima.
Waandishi wa habari, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa, alipokuwa akizungumza nao, kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mikopo hiyo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu jijini jana.
Wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua matukio na maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa, wakati wa mkutano huo jijini jana.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa, akitoa ufafanuzi wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Urejeshwaji Mikopo, Juma Chagonja na kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi-Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Veneranda Malima.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa, akijibu, maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Urejeshwaji Mikopo, Juma Chagonja.
1.0
UTANGULIZI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilipoanzishwa
mwaka 2005 pamoja na utekelezaji wa Sera ya Uchangiaji, ilipewa majukumu mawili
makubwa; kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na kurejesha mikopo kutoka kwa
wanufaika wa mikopo hiyo ili kuufanya mfuko wa mikopo ya elimu kuwa endelevu.
Mikopo ya wanafunzi ilianza kutolewa mwaka
1994/1995 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu
ya Juu, Sayansi na Teknolojia. Wakati huo serikali ilikuwa haikusanyi madeni
kutoka kwa wanufaika hadi Bodi ilipoanza kufanya kazi.
Kampeni za urejeshaji mikopo zilianza rasmi
mwaka 2006/2007, na tangu wakati huo kumekuwa na mafanikio makubwa katika
ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya
juu.
1.1
Mikopo iliyotolewa
Jumla ya Sh. 1,807,223,411,221.00
zimekopeshwa kwa wanafunzi kati mwaka wa masomo 1994/1995 na mwezi Juni,
2014. Kati ya hizo, Sh. 51,103,685,914 zilitolewa
na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia na kiasi kilichobaki
cha Sh. 1,756,119,725,307.00
kimetolewa na Bodi ya Mikopo tangu mwezi Julai, 2005 ilipoanza kazi rasmi.
1.2 Urejeshaji wa mikopo
Kiasi cha mikopo kilichokwishaiva na hivyo
kuwa tayari kwa marejesho ni jumla ya Sh.
833,476,985,770.75 hadi kufikia tarehe 28 Februari, 2015. Kati ya fedha hizo, mikupuo iliyokuwa tayari
kurejeshwa ni kiasi cha Sh. 123,828,003,422.67. Kiasi cha mikopo
kilichokuwa kimekusanywa kutoka kwenye mikopo iliyoiva ni Sh. 65,275,252,446.49 ambazo ni sawa na asilimia 53 ya
mikupuo iliyokuwa tayari kurejeshwa hadi kufikia tarehe
28 Februari, 2015.
Aidha, jumla ya Wadaiwa 136,198 (sawa na asilimia 76.94 ya wadaiwa wote 177,017
ambao mikopo yao imeiva) wametambuliwa na wanaendelea na marejesho ya mikopo
hadi tarehe 28 Februari, 2015.
Jedwali 1: Takwimu za Urejeshaji wa Mikopo ya
Wanafunzi
Mwaka
|
Urejeshaji kwa mwaka (Tzs)
|
Jumla (Tzs)
|
2006/2007
|
53,616,011.22
|
53,616,011.22
|
2007/2008
|
858,941,262.29
|
912,557,273.51
|
2008/2009
|
1,176,404,180.00
|
2,088,961,453.51
|
2009/2010
|
2,147,075,264.78
|
4,236,036,718.29
|
2010/2011
|
4,409,171,729.99
|
8,645,208,448.28
|
2011/2012
|
11,508,714,785.96
|
20,153,923,234.24
|
2012/2013
|
14,850,247,552.21
|
35,004,170,785.45
|
2013/2014
|
18,088,801,344.43
|
53,092,972,129.88
|
1.3 Tozo la
Utunzaji wa thamani ya mikopo
Hadi sasa, mikopo yote inayotolewa na Bodi kuanzia mwaka
wa masomo 1994/1995 inabeba tozo la utunzaji wa thamani ya mikopo (value
retention fee) kwa asilimia 6 kwa
mwaka, kwa kiasi chote cha mkopo ambacho hakijarejeshwa.
2
MIKAKATI YA UREJESHAJI WA MIKOPO NA CHANGAMOTO
ZILIZOPO
2.3
Mikakati ya Urejeshaji mikopo
Bodi inaendelea kuongeza kasi ya urejeshaji wa mikopo kwa
kubuni mikakati kadhaa ikiwa ni pamoja na:
(i)
Kuendelea
kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kurejesha mikopo
(ii)
Kuongeza
matumizi ya mitandao ya simu (M-pesa/Airtel Money) katika kukusanya madeni.
(iii)
Kuzidisha ushirikiano zaidi na wadau muhimu
hasa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mamlaka ya Mapato, Waajiri, Sekta isiyo rasmi
na Wanufaika wa mikopo.
(iv)
Kuchukua
hatua za kisheria dhidi ya Wanufaika wanaokaidi kurejesha mikopo yao. Hadi sasa
kuna kesi 18 zilizofunguliwa mahakamani dhidi ya wadaiwa sugu.
(v)
Kutumia mfumo wa “LAWSON” katika kubaini
Wadaiwa na kukusanya madeni kutoka kwa
Waajiriwa wa Serikali.
(vi)
Kushirikiana na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Heasbu za Serikali katika kuhakiki uwajibikaji wa Waajiri katika kutekeleza
wajibu wao katika urejeshaji wa mikopo.
2.2 Changamoto zilizopo na mikakati ya kukabiliana nazo
(i)
Imani potofu kwamba mikopo
inayotolowa na Bodi ni ruzuku
Bado kuna baadhi ya Wadau wenye imani potofu kuwa
fedha zitolewazo na Bodi ni ruzuku. Imani hii potofu inazorotesha juhudi za
ukusanyaji wa madeni na inachangia ongezeko la waombaji wa Mikopo hata wale
ambao wana uwezo wa kujigharamia.
Mkakati wa kukabiliana na changamoto hii ni kwa Bodi
kuendelea kuelimisha umma na kuongeza jitihada za ukusanyaji madeni ili
kusisitiza ujumbe kwamba hii ni mikopo ni si ruzuku.
(ii)
Kukosekana
kwa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa baadhi ya Wadau
Baadhi ya Wadau hasa waajiri na
Wadaiwa hawawajibiki ipasavyo kwa mujibu wa Sheria katika kurejesha mikopo, kusaidia kuwatambua na
kuwasilisha taarifa za wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.
Mkakati wa kukabiliana na changamoto hii ni kwa Bodi kuendelea
kuwaelimisha waajiri na umma kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kushirikiana na Bodi
katika zoezi la kurejesha Mikopo.
2.4
Hitimisho
Kwa Taarifa hii,
Bodi inawasisitizia wanufaika wa Mikopo, wazazi/walezi, waajiri na umma kwa
ujumla kutambua kuwa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ni sehemu ya
utekelezaji wa Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya Juu. Hivyo ni muhimu kushirikiana
katika kufanikisha marejesho ya mikopo iliyoiva ili kuuwezesha mfuko wa
ukopeshaji kuwa endelevu na kutoa nafasi kwa wahitaji wengi zaidi kunufaika na
mikopo ya elimu ya juu.
Imetolewa
na:
KITENGO
CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
No comments:
Post a Comment