Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga
akizungumza na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
waliofika ofsini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba
yao ya mafunzo kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Bihigwe leo mjini Kasulu.
Katikati ni Mkuu wa msafara huo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa na
wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana wa wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu
Bw. Bernard Ntikabuze (kushoto) akiagana
na akipeana mkono na Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga wakati walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi huyo leo.
Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bw. Muguha Titus
Muguha akizungumza na Vijana wanaoshiriki mafunzo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (hawapo pichani) yanayotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo. Kutoka kulia ni Afisa Vijana wa Wizara hiyo Bi.
Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bibi. Esther Riwa, Mkuu wa
Kituo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mbeya Bw. Laurian Massele na
Afisa Vijana wa Mkoa wa Kigoma Bw. Edward Manase
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada kuhusu
Sera ya Maendeleo ya Vijana na Stadi za Maisha kwa baadhi ya Vijana wa
Halmashauri za Kasulu na Buhigwe leo
katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Wilayani Kasulu.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada kuhusu
Sera ya Maendeleo ya Vijana na Stadi za Maisha kwa baadhi ya Vijana wa
Halmashauri za Kasulu na Buhigwe leo
katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Wilayani Kasulu.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada zilizokuwa
zilizokuwa zikiwasilishwa na Mkuu Mkuu
wa Kitengo cha Sheria Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Bibi. Esther Riwa haypo pichana leo mjini Kasulu.
Ofisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa maada kuhusu Mwongozo wa Mkopo wa
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Wilayani Kasulu wakati wa mafunzo kwa Vijana
wa Halmashauri za Kasulu na Buhigwe.Jumla ya Vijana 66 wamehudhuria mafunzo
hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu
Bw. Bernard Ntikabuze akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo walipofika ofisini kwake ili kujitambulisha kabla ya
kuendelea na ratiba ya mafunzo na
ukaguzi wa miradi Wilayani hapo leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga (watatu
kutoka kulia kabla ya mabadiliko) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake
leo. Kutoka kulia ni Afisa Utamaduni na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kasulu Bw. Mbogo, Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa na Afisa Vijana wa Mkoa
wa Kigoma Bw. Edward Manase. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)
No comments:
Post a Comment