TANGAZO


Saturday, February 21, 2015

UN:Wanaoendesha uhalifu Syria kutajwa

Wanaoendesha uhalifu nchini Syria sasa kutajwa na umoja wa mataifa
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanapanga kuchapisha majina ya takriban watu 200 wanaotuhumiwa kuendesha uhalifu wa kivita nchini Syria.
Tume huru ya uchunguzi ya umoja wa mataifa inasema kuwa kumekuwa na ongezeko la uhalifu nchini humno.
Majina yanayojumuisha wakuu wa kijeshi , wasimamizi wa magereza na makamanda wa makundi yasiyokuwa ya serikali yaliyo na silaha tayari yamewasilishwa kwa tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa.
Serikali ya Syria hatahivyo imekataa kutoa ushirikiano kwa tume hiyo.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 220,000 wameuawa nchini Syria na mamilioni ya wengine wamehama makwao wakati wa mazozo wa miaka minne .

No comments:

Post a Comment