TANGAZO


Saturday, February 21, 2015

B Haram lawaua watu 21 likitoroka vita

Wapiganaji wa Boko Haram
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa takriban watu 21 wameuawa na wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wakirudi nyuma katika eneo lililo kaskazini masharki mwa nchi.
Kiongozi mmoja katika jimbo la Borno amesema kuwa wanamgambo hao walichoma vijiji kadha karibu na mji wa Chibok .
Msemaji wa jeshi la Nigeria alisema kuwa waasi hao walikuwa wakikimbia mashambulizi ya ardhini na ya angani ya jeshi la Nigeria katika msitu wa Sambisa.
Wakuu wa majeshi kutoka Nigeria na mataifa manne majirani wa Nigera wakiwemo Chad, Niger , Cameroon na Benin watakutana wiki ijayo kukamilisha mikakati ya kampeni ya ardhini ambayo itawajumuisha wanajeshi 8700 dhidi ya Boko Haram.

No comments:

Post a Comment