TANGAZO


Saturday, February 21, 2015

Ebola:Liberia sasa kufungua mipaka yake

LIberia imesema kuwa itafungua mipake yake baada ya kuudhibiti ugonjwa wa ebola
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf anasema kuwa mipaka ya nchi yake itafunguliwa kesho Jumapili baada ya kufungwa mwaka uliopita kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola.
Kwenye taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wake rais Sirleaf alisema kuwa amri za nchi nzima za kutotembea nazo pia zitaondolewa.
Alisema kuwa serikali itahakikisha kuwa hatua zimewekwa kuzuia ugonjwa wa ebola kuingia nchini humo kupitia kwa vifuko vyote vya mipaka ya nchi hiyo.
Liberia ni moja ya nchi tatu za Afrika magharibi kati ya Sierra Leone na Guinea iliyoathirika vibaya na ugonjwa wa ebola lakini hatahivyo imefanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo
Ugonjwa wa ebola umewaua zaidi ya watu 9000 magaharibi mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment