Hapa moja ya vikundi vya Dufu kikitumbuiza katika Maulidi hayo. Na chini ni picha za matukio mbalimbali kwenye Maulidi hayo.
Mzee Mwinyi akiwa na baadhi ya viongozi wa Dini ya Kiislamu nchini.
Kikundi cha Dhikri kutoka Kondoa kikiwa kazini katika kumdhukuru Mwenyezi Mungu (S.W) kwenye Maulidi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu (kulia), akiwa na baadhi ya wageni na Mkurugenzi wa Stuftung.
Umati wa waumini wa Dini ya Kiislamu ukiwa katika Maulindi hayo.
Kadhi Mkuu akiomba dua pamoja na Mzee Mwinyi (kulia) katika Maulidi hayo.
Waumini wakiwa katika dua kwenye Maulidi hayo.
Moja ya kikundi cha Dufu kikitumbuiza kwenye Maulidi hayo.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akizungumza kwenye Maulidi hayo.
Kikundi cha Dhikri kikiwa kazini.
Mmoja wa Maustaadhi akisoma Malngo wa Nne wa Maulidi hayo.
Na Joseph Mabula
RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi amesema Uislamu unaeleza wazi kuwa kuua ni dhambi kubwa huku akiwataka waislamu kuendelea kuilinda amani iliyopo nchini na kutoshawishika na watu wasioitakia mema nchi yetu.
Hayo aliyasema Dar es salaam juzi, wakati wa maulidi ya kumbukumbu ya kuzaliwa mtume mohamed ambapo alisema amani ni tunu aliyotupa mwenyezi mungu hivyo tuilinde kwa njia yoyote na tusiruhusu mtu aichezee amani yetu.
"Ndugu zangu waislamu mliokuwa hapa na msio waislam,tuilinde amani yetu,tuilee amani yetu,tuwe na uvumilivu,sio kila usilolipenda ulichukulie hatua.
Leo wenzetu katika dunia hii wanauawa kwa mafungu,lakini uislamu unasema kuua ni dhambi kubwa"alisema Mwinyi.
Katika hatua nyingine Rais mstaafu Ali Hassan mwinyi alizindua kitabu kinachozungumzia uchumi kwa waislamu.
Naye Sheikh mkuu wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salim alisema waislamu wengi wamekuwa wakikosa fursa za kiuchumi kutokana na taasisi nyingi za fedha kudai riba.
"Dini ya kiislam hairuhusu riba, kwao riba ni haramu hivyo kitabu hicho walichokizindua kinatoa somo kuhusu kuimarisha uchumi,"alisema.
Wakati huohuo Shikh huyo aliwataka watanzania kuchanga fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu Mwinyi ili agombee tena uraisi.
No comments:
Post a Comment