Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa Msikiti Mpya wa Kijiji cha Kiongoni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa Kusini, Dk. Idriss Muslim Hijja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuufungua Msikiti Mpya wa Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja na kuanza rasmi shuhuli za Ibada. kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa Kusini, Dk. Idriss Muslim Hijja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa nne kushoto) pamoja na Mashekhe na Viongozi na Waislamu mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada ya Swala ya Adhuhuri, iliyoongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji (kulia) baada ya ufunguzi wa Msikiti Mpya katika Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) pamoja na Mashekhe na Viongozi na Waislamu mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada ya Swala ya Dhuhuri iliyoongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji (hayupo pichani) baada ya ufunguzi wa Msikiti Mpya katika Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar Dk. Sheikh Muhidin Siasa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa Msikiti mpya wa Kijiji cha Kiongoni Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein azungumze na waislamu baada ya ufunguzi wa Msikiti Mpya katika Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Waislamu wa Kijiji cha Kiongoni Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kuufungua Msikiti mpya kijijini hapo leo uliojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe, Haroun Ali Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akizungumza na Waislamu wa Kijiji cha Kiongoni Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kuufungua Msikiti mpya kijijini hapo leo uliojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe, Haroun Ali Suleiman.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein amefungua
msikiti wa Kiongoni Makunduchi na kutoa nasaha zake kwa Waumini kuwa Msikiti ni
nyumba ya Mwenyezi Mungu hivyo itumike kuwaunganisha waumini na sio kuwatenganisha
au kuwagombanisha.
Alhaaj Dk. Shein
alisema kuwa haitokuwa vyema kusikia mizozo ikiwa ni pamoja na kugombania
uongozi wa msikiti miongoni mwa viongozi au Waislamu katika misikiti kwa sababu
mbali mbali kwani matokeo hayo yatakuwa ni kinyume na malengo na azma ya
kuuimarisha misikiti na kutozitumia vyema neema za Mwenyezi Mungu.
Alisema kuwa
licha ya kuwa baadhi ya wakati wapo wanaokhafilika na kufanya hivyo ambapo
Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa imani yake ni kuwa waumini watafuata nyayo za
mashehe na Maulamaa waliopita katika kufuata matendo mema
Aidha, Dk. Shein
alisisitiza kuwa msikiti huo pamoja na madrasatul alizozifungua ziwe ni
chemchem ya elimu mbali mbali ikiwa ni pamoja na usomaji Kuran, Fikhi na
taaluma nyengine za dini, malezi na imani.
Alhaj Dk. Shein
alisema kuwa Kiongoni imetoa watu mbali mbali wenye maarifa makubwa kama
marehemu Mzee Sheikh Idrisa Abdul Wakil ambaye alitoa mchango mkubwa katika
maendeo ya nchi na sio wananchi wa Kiongoni na Makunduchi pekee yake bali wa
Taifa zima.
Sambamba na hayo,
Dk. Shein aliwasisitiza waumini kuendelea kuhimizana juu ya umuhimu wa
kuendeleza amani iliyopo kwa manufaa yao na vizazi viliopo na kuwataka wazazi
kutochoka kusimamia malezi ya watoto na kuwaelekeza katika maadili mema sambamba
na mienendo inayozingatia utamaduni na mafundisho ya dini.
Alhaj Dk. Shein
alisema kuwa ujenzi wa msikiti na madrasa ni masuala ya kheri na yenye umuhimu
katika kuuendeleza Uislamu. Mapema kabla ya ufunguzi wa Msikiti huo, Alhaj Dk.
Shein alifungua madrasatul Tawheed iliyopo hapo hapo Kiongoni Makunduchi.
Nae Mkuu wa Mkoa
wa Kusini kwa niaba ya Wananchi wa Makunduchi walitoa shukurani kwa Alhaj Dk.
Shein kwa kushiriki kikamilifu katika
uzinduzi wa Madrasa pamoja na msikiti kwa nyakati tofauti katika kijiji hicho
cha Makunduchi na kusisitiza haja ya kuitumia vizuri misikiti hiyo pamoja kuidumisha
ili iwaneemeshe waumini na Uislamu kwa jumla.
Nao wanakijiji
cha Kiongoni wakisoma risala yao walieleza kuwa wazo la kujenga msikiti huo
lilitolewa kiasi cha miaka 110 iliyopita kutoka kwa mababu zao na kuishukuru
familia ya Bwana Ali Kitambo kwa kukubali kutoa ardhi yao kuwa ni Wakfu.
Walieleza kuwa
baada ya kijiji hicho kupanuka msikiti huo uliendelea na ujenzi kwa msaada wa
mfadhili Sheikh Mwinyi Mohamed Kitovu na baadae ulifanyiwa matengenezo na
marehemu Sheikh Idrisa Abdulwakil pamoja na Sheikh Ibrahim Ali Suleiman na
Sheikh Mustafa Ali Suleiman.
Baada ya hapo
walisema kuwa mnamo mwaka 2013, Mhe. Mwakilishi wa Jimbo hilo la Makunduchi nae
aliomba kuufanyia matengenezo zaidi na ndipo wanakijiji hao wakamuomba
kuuzidisha msikiti huo ili uwe mkubwa zaidi.
Nae Mkuu wa Chuo
cha Kiislamu Dk. Muhidin Siasa akitoa mawaidha katika hafla hiyo ya ufunguzi wa
msikiti alieleza kuwa Makunduchi ni kitovu kikubwa cha Mashehe, na Maulamaa mbali
mbali hivyo ipo haja ya kuendeleza utamaduni huo.
Wakati huo huo, Alhaj Dk. Shein alizindua Madrasatul Muzdalifa
Al-Qadiria Shafii, huko Mzuri Makunduchi na kueleza kuwa kuna haja ya
kuimarisha mashirikiano baina ya wazazi, walimu na na jamaii yote kwa jumla katika kuwaepusha
watoto na wanawake katika vitendo vya udhalilishaji.
Alisema kuwa
jukumu la kuwalinda watoto na wanawake ni la watu wote na kusisitiza kuwa
vitendo vya udhalilishaji wa watoto ni kinyume na maadili na haki za binaadamu hivyo haipaswi kufumbiwa
macho kwani vinatoa taswira mbaya kwa
jamii na mustakbali wa maisha ya watoto.
Alhaj Dk. Shein alisema
kuwa Serikali kwa kushirikiana na Taasisi na Mashirika mbali mbali imeanzisha Kampeni ya miaka miwili ya kupambana
na ukatili dhidi ya akina mama na watoto.
Kutokana na elimu
zote zinatokana na Mwenyezi Mungu Alhaj Dk. Shein aliwanasihi wazazi na walezi
kuwahimiza vijana kufuata na masomo ya skuli kwani Serikali imekuwa ikichukua
jitihada za makusudi katika kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya elimu huku
pia, Serikali ikiimarisha mazingira ya skuli zote za Zanzibar.
Nae Mwakilishi wa
Jimbo la Makunduchi ambaye pia, ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman
alisema kuwa mafanikio ya ujenzi huo wa
Madrasa ya ghorofa moja umetokana na mashirikiano mazuri ya mfadhili na wananachi
wa eneo hilo kupitia Kamati yao iliyo chini ya Mwenyekiti wake Mzee Makame Mudu.
Akisoma risala
kwa niaba ya wa madrasa hiyo, Ustadh Ali Habib Suleiman alisema kuwa Madrasa
hiyo imeanzishwa mnamo mwaka 1940 ambapo
baadae ikaendelezwa na
Mwalimu Bi
Atamani binti Ali ambaye sasa ni marehemu kwa mashirikiano na Ustadhi Ramadhan
Mwinyi hadi kupata mfadhili mnamo mwaka
2013 na 2014 ujenzi ulikamilika ambao umegharimu Shilingi za Kitanzania Milioni
37.
Sambamba na hayo,
Dk. Shein aliwataka wazazi na walezi kushirikiana na waalimu katika kufuatilia
masomom ya watoto pamoja na mienendo yao ili kuwaepusha na utoro na kuacha
vitendo viovu.
Nae Kadhi Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Khamis Haji alitoa shukurani kwa niaba ya Ofisi yake kwa
mfadhili wa Madrasa hiyo na kusisitiza kuwa viongozi wa dini wanapaswa
kuendelea na jitihada zao katika kutoa elimu bora ya dini kwa vijana.
Aidha, Dk. Shein
alikubali ombi la madrasa hiyo la kuwapatia kompyuta moja pamoja na printa yake
huku akiwaahidi kuwaunga mkono pale
watakapokuwa tayari kuanza ujenzi wa nyumba ya mwalimu mkuu wa Madrasa hiyo
pamoja na kuanza skuli ya maandalizi ndani ya Madrasa hiyo kama walivyoomba
katika risala yao.
No comments:
Post a Comment