TANGAZO


Friday, February 20, 2015

Mlipuko wa bomu wawaua watu 30 Libya

libya
Zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine kujeruhiwa kutokana na bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari huko Libya katika mji wa mashariki wa Qubbah.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye gari yalilenga kituo cha mafuta na jengo la usalama katika mji huo.
Hakuna aliyejitangaza kuhusika na shmbulizi hilo .
Libya imo katika hali ya mtafaruku kwa miaka minne sasa tangu kupinduliwa kwa aliyekuwa kiongozi wake Muammar Gaddafi huku kukiwa na serikali mbili na mabunge mawili ambayo yanapigania uongozi.

No comments:

Post a Comment