TANGAZO


Friday, February 20, 2015

Oxfam:Watu 50,000 wametoroka Darfur

Baadhi ya watoto ambao wazazi wao wamelitoroka eneo la Darfur
Shirika la wahisani la Oxfam limesema kuwa zaidi ya watu elfu hamsini kutoka eneo la Darfur huko Sudan wamekimbia makazi yao tangu mwaka uanze.
Linasema watu wanaokimbia mapigano yaliyozuka upya wanaishi katika maeneo ya wazi na wanaobahatika wanakaa chini ya miti.
Baadhi ya familia zilipoteza watoto wake njiani.
Baadhi ya wanawake katika eneo la Darfur.zaidi ya watu 50,000 waleitoroka eneo hilo mwaka huu pekee
Chakula, mifugo na mali nyingine imeporwa vijijini.
Mzozo huo wa Darfur umekuwa ukiendelea kwa karibu miaka kumi na miwili.
Kumekuwa na mikataba mingi ya amani kati ya serikali na makundi mbalimbali ya waasi lakini imekuwa ikiporomoka baada ya kutiwa saini.

No comments:

Post a Comment