TANGAZO


Friday, February 20, 2015

Maafisa wa serikali wauawa Mogadishu

Hoteli yashambuliwa mjini Mogadishu Somalia
Watu wengi wakiwemo maafisa wakuu wa serikali wameuawa na wengine kujeruhiwa kutokana na mashambulizi mawili ya bomu katika hoteli moja katika mji mkuu wa Somali Mogadishu.
Mawaziri wawili wamearifiwa kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la Al Shabaab -- yalifanyika leo ijumaa wakati wa maombi.
Mwandishi wa BBC aliyeko Mogadishu anasema kuwa mlippuaji wa kujitolea muhanga alijilipua ndani ya chumba kimoja cha kufanyia maombi katika hoteli hiyo.
Shambulizi jingine lilitokea kwenye gari lililokuwa limeegeshwa nje ya chumba.
Al Shabaab imeiambia BBC kuwa ilihusika katika shambulizi hilo kwa sababu wafanyikazi wa serikali walikuwa wasaliti.

No comments:

Post a Comment