TANGAZO


Thursday, February 19, 2015

Aliyekuwa waziri mkuu Thailand ashtakiwa

Aliyekuwa rais wa Thailand Yingluck Shinawatra
Aliyekuwa waziri mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ameshtakiwa katika mahakama ya juu kwa kosa la kutowajibika kwa kuhusika kwake katika mpango wa ruzuku ya mchele uliogubikwa na mzozo ulioidhinishwa na serikali yake.
Bi. Yingluck, ambaye utawala wake uliondoshwa kufuatia mapinduzi ya jeshi mwaka jana, tayari ametimuliwa na kupigwa marufuku kutoshiriki siasa kwa miaka mitano.
Mwezi mmoja baada ya kutimuliwa kwake na bunge lililoteuliwa na jeshi, sasa Yingluck Shinawatra anakabiliwa na kesi ya uhalifu ambayo huenda akipatikana na hatia na kahukumiwa hadi miaka kumi gerezani.
Wafuasi wake wanalalamika kwamba ni mashtaka ya kisiasa yanayonuiwa kumharibia jina kiongozi huyo aliyechaghuliwa kwa kura nyingi.
Wanataja kwamba hakuna makosa yoyote ya rushwa yaliothibitishwa dhidi ya mpango huo wa ruzuku na kueleza kwamba ni hatua yenye nia safi kuwasiaida wakulima.
Lakini serikali ya kijeshi imetupilia mbali wasiwasi huo na kuonya kwamba Bi. Yingluck asijaribu kutorokea katika nchi za nje kama alivyofanya kakake Thaksin miaka sita iliyopita baada ya yeye pia kushtakiwa.
Serikali inatafakari pia kumshtaki kwa gharama nzima ya ruzuku hiyo ambayo inasema inagharimu dola bilioni kumi na nane.
Huku sheria inayotumika ikiwa bado ni ya kijeshi,huenda pasiwepo maandamano yoyote ya kupinga namna anavyotendewa Yingluck.
Lakini masaibu yake yanasukuma zaidi ahadi ya jeshi kuidhinisha upatanishi liliyotoa wakati lilipoipindua serikali mwaka jana.

No comments:

Post a Comment