TANGAZO


Thursday, February 19, 2015

Taifa la Niger laomboleza mauaji

Rais wa Niger Issoufour
Baada ya kisa cha kulipuliwa kwa kijiji kimoja nchini Niger, sasa serikali ya nchi hiyo imetangaza siku tatu za maombolezi.
Serikali inasema kuwa ni kumbukumbu ya kitaifa dhidi ya wanakijiji 37 waliouawa baada ya ndege kushambulia kijiji chao.
Serikali ya Niger, imeanzisha uchunguzi kubaini ni ndege ya aina gani na nia ya kuwalipua wana kijiji hao ilikuwa ni nini.
Kijiji hicho kilicholengwa cha Abadam kiko karibu na mpaka na Nigeria.
Wahasiriwa walikuwa katika sherehe za mazishi pale waliposhambuliwa wakidhaniwa kuwa ni wapiganaji wa Boko Haram.
Jeshi la Nigeria limekataa kuwa ndege yake ilihusika.
Mataifa ya ukanda huo yameanzisha mashambulio makali dhidi ya kundi hilo la itikadi kali la Boko Haram.

No comments:

Post a Comment