TANGAZO


Thursday, February 19, 2015

Libya yaitaka UN kuiruhusu Kununua silaha

Libya yataka UN kuiruhusu kununua silaha
Waziri wa mambo ya nje wa Libya, Mohamed Daree ametoa wito kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo vya kununua silaha vilivyowekwa mwaka wa 2011.
Amesema jamii ya kimataifa, inahitaji kuchukua msimamo dhabiti ili kuisaidia kujenga na kuimarisha uwezo wa jeshi lake.
Amesema ni kitendo halali na inayohitajika kwa jamii ya kimataifa kuipa misaada ya dharura.
Waziri huyo ameongeza kusema kuwa endapo hatua hiyo haitachukuliwa basi wapiganaji wa Islamic State
watakuwa na ushawishi mkubwa na huenda hali ya usalama nchini humo ikasambaratika zaidi.
Libya yataka UN kuiruhusu kununua silaha
Misri pia imetoa wito huo huo wa kuiondolea Libya vikwazo vya kununua silaha na wakati huo huo kutaka jamii ya kimataifa kuzuia meli zinazosafirisha sheheza za silaha hadi Libya kwa makundi ya kigaidi.
Nchi hizo mbili zimesitisha wito wao wa kuitaka umoja wa mataifa kutuma vikosi vyake nchini Libya kupambana na wapiganaji wa ISIS.
Kwa sasa jamii ya kimataifa haina nia ya kutuma kikosi chochote cha ardhini Libya kutokana na sababu za kiusalama.
Lakini mabalozi wa mataifa ya magharibi ambao wamekuwa wakishinikiza kuwepo kwa mazungumzo ya amani yatakayoongoza
na umoja wa mataifa ili kubuniwe serikali ya muungano wa kitaifa nchini Libya, wameelezea wasi wasi wao kuhusiana na ombi hilo la Libya la kutaka vikwazo hivyo kuondolewa.
Mabalozi hao wanasema huedna silaha hizo zikaishia mikononi mwa makundi ya wanamgambo wa kiislamu na hivyo kuhatarisha usalama zaidi.

No comments:

Post a Comment