*Safari hii ni katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar
*Yapigwa 1-0, Uwanja wa Aman mjini Zanzibar
Wachezaji wa timu ya Simba wakipasha moto misuli kabla ya kukaguliwa na Mgini Rasmin Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo ilioaza jana mchana Uwanja wa Amaan Zanzibar. (Picha zote kwa hisani ya Zanzinews blog)
Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sigar wakipasha moto misuli kabla ya kukaguliwa na Mgini Rasmin Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo ilioaza jana mchana, Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Kamisaa wa Mchezo huo Musin Kamara, wakati wa uzinduzi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi yaliozinduliwa jana mchana na Balozi Seif, katika uwanja wa Amaan.
Makamu wa Pili wa Rais wac Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaan usiku wa kuamkia leo.
Makamu wa Pili wa Rais wac Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sigar, kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaan usiku wa kuamkia leo.
Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaam. Timu ya Mtibwa imeshinda bao 1--0
Kikosi cha Simba kilichokubali kipigo cha Bao moja kwa mara ya pili mchezo wa mwazo na Mtibwa Simba wamefungwa mabao 4--2, na usiku wa kuamkia leo wamekubali tena kuwa wateja wa Mtibwa kwa kufungwa bao 1--0.
Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar kilichotoka kifua mbele dhidi ya ushinda wa Bao 1--0 dhidi ya timu ya Simba wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika usiku huu uwanja wa Amaan Zanzibar.
Elias Maguri wa Simba akikokota mpira.
Kessy wa Simba, akimiliki mpira.
Kessy wa Simba akipiga krosi kuelekea langoni kwa Mtibwa.
Kocha mpya wa Simba (kulia), akizungumza jambo na mmoja wa viongozi wa Simba akiwa jukwaani wakati wa mchezo huo usiku wa kuamkia leo.
Kocha mpya wa Simba (kulia), akikuna kichwa baada ya kuiona timu hiyo ikikubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar.
Kocha wa timu ya Yanga, akiwa na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa (kulia), wakijadili jambo wakati wa mchezo huo.
Na Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar
TIMU Simba ya Dares salam imeyaaanza vibaya mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea mjini hapa baada ya kukubali kipigo cha 1 – 0 kutoka kwa Mtibwa Sugar ya Morogoro, lililofungwa na Henry Joseph Shindika katika dakika ya 44 ya mchezo huo usiku wa kuamkia leo, Uwanja wa Aman mjini Zanzibar.
Joseph ambaye kwa vipindi tofauti aliwahi kuichezea Simba kabla ya kujiunga na wakata miwa hao, alifunga goli hilo baada ya kupokea pasi ya Ame Ali ‘Zungu’ ambaye alipokea mpira wa kona iliyochongwa na Ally Lundenga kutoka mashariki ya uwanja lakini kutokana na kuwa katika mazingira magumu alitoa pasi kwa mfungaji, aliyekuwa mbele yake naye bila kusita akausukumia wavuni mpira huo na kuandika bao kwa timu hiyo.
Goli hilo liliibua shamra shamra za mashabiki kadhaa wa Mtibwa Sugar, waliokuwa wakisaidiwa na mashabiki wa Yanga na kuufanya mchezo huo, kuwa na msisimko zaidi ya michezo mingine miwili iliyochezwa awali katika siku hiyo.
Kabla ya kufungwa kwa goli hilo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu huku Simba ikikosa nafasi kadhaa za wazi, ikiwemo katika dakika 25 za awali ambapo washambuliaji wake Elius Maguri, Ibrahim Ajib na Abdi Banda waliweza kulifikia lango la Mtibwa na kushindwa kutumia vyema nafasi walizozipata baada ya mipira waliyoelekeza langoni kwa wapinzani wao kuokolewa na walinzi au kudakwa na golikipa wa Mtibwa, Said Mohamed ambaye alikwa nyota wa mchezo huo.
Hali hiyo pia ilikuwa kwa Mtibwa ambayo ilionekana kutulia na kufanya mashambulizi zaidi kuanzia dakika ya 30 huku Joseph, Ame Ally na Ibrahim Rajab ‘Jeba’ wakishindwa kufunga kutokana na nafasi walizozipata.
Hali hiyo ya kosa kosa iliendelea hata baada ya kipindi cha kwanza kukamilika huku mtibwa inayofundishwa na nahodha wa zamani wa timu ya Taifa Stars Mecky Mexime ikionekana kuimarika zaidi hasa katika kiungo na kusababisha mashambulizi mengi ambayo hayakuzaa matunda.
Licha ya kupoteana katika baadhi ya wakati katika kipindi cha pili simba iliyokuwa chini ya kocha msaidizi wa timu hiyo suleimani matola ililisakama lango la mtibwa katika dakika za mwisho mwisho za mpambano huo ambao pia ulishuhudiwa na kocha mpya wa timu hiyo Mserbia Goran Kapunovic ‘Kapu’ aliyekuwa jukwaani sambamba na kocha wa Yanga Hans van Der Plujin na msaidizi wake Charles Mkwasa.
Mchezo huo ambao ulikuwa maalum kwa ufunguzi wa mashindano hayo uliofanywa na Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi, katika kuhakikisha zinapata matokeo mazuri timu zote mbili zilifanya mabadiliko kwa Simba iliyokuwa ikicheza bila ya nyota wake wanne wa kigeni kuwatoa Ibrahimu Ajib mnamo dakika ya 56 na nafasi yake kuchukuliwa na Danny Sserenkuma huku Said Ndemla akimpisha Jonas Mkude katika dakika ya 81.
Kwa upande wa Mtibwa Jamal Mnyate aliyeoneshwa kadi ya njano na mwamuzi wa mchezo huo Mfaume Ali kwa mchezo mbaya dhidi ya Shaaban Kisiga sawa na Hassan Keisy wa Simba aliyemchezea vibaya Ibrahim Rajab ‘Jeba’, alitolewa mnamo dakika ya 61 na nafasi yake kuchukuliwa na Vicent Barnabas, Mussa Hassan ‘Mgosi’ aliingia kuchukua nafasi ya Ame Ally huku Ramadhani Kichuwa akiingia kuchukua nafasi ya ‘Jeba’ aliyeumia na kushindwa kuendelea na mchezo huo katika dakika ya 72.
Wakizungumzia mchezo huo makocha wa timu zot mbili waliwapongeza wachezaji wao kwa kuonesha mchezo mzuri licha ya kutokuwa makini katika kufunga jambo lililopelekea kukosekana kwa nafasi nyingi za kufunga.
“Kufungwa ni sehemu ya mchezo lakini namini kukosekana kwa umakini na utulivu kwa wachezaji wangu ndiko kulikopelekea matokeo haya jambo ambalo namini linarekebishika”, alisema Suleiman Matola kocha msaidizi wa Simba.
Nae kocha Mexime wa Mtibwa alisema, “bado kuna kazi ya kufanya kwani licha ya kushinda mchezo huu bado kuna mambo hayako sawa hasa katika kumalizia. Tuna malengo ya kulitwaa taji hili lakini pia kuendelea kufanya vyema katika ligi hivyo ni lazima tufanyie kazi kila dosari inayojitokeza”.
Timu hizo ambazo zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara katika kipindi cha miezi miwili iliyopita zilikutana mara tatu huku Mtibwa ikiibuka na ushindi mara mbili ukiwemo mchezo wa juzi na ule wa kirafiki kati ya timu hizo uliochezwa Disemba katika uwanja wa azam Complex uliomalizika kwa Simba kulala kwa mabao 4 – 2 katika mchezo wa kirafiki baada ya kutoka sare ya 1 – 1.
Katika mchezo wa mapema makamo bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar timu ya polisi ilimaliza dakika 90 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya shaba f. c lililofungwa na ali kwa kichwa na ali Khalid mnamo dakika ya 36 baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Mwita Makame.
No comments:
Post a Comment