Gwiji la Muziki wa Kizazi Kipya, Profesa J. akiwapagawisha mashabiki waliofika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kushuhudia Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika jijini Dar es Salaam mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.
Gwiji la Muziki wa Kizazi Kipya, Profesa J. akiwapagawisha mashabiki waliofika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kushuhudia Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika jijini Dar es Salaam mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki, akipanda jukwani kuwaburudisha mashabiki wake waliofurika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la “Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika jijini Dar es Salaam,Mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki, akiwapagawisha mashabiki wake waliofurika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika jijini Dar es Salaam,Mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wamefurika katika Ufukwe wa Bahari
Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika
jijini humo mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuakaribisha Mwaka 2015 jana.
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Profesa
J wamepagawisha mamia ya wapenzi wa muziki huo katika tamasha la
wazi la kukaribisha mwaka mpya la”Vodacom maisha ni murua” lililofanyika katika
ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam jana.
Mbali na Profesa J,wanamuziki
Temba,Mkatoliki nao walikonga nyonyo za washabiki.
Mwanamuziki wa kwanza kupanda jukwaani ambaye alipagawisha wapenzi
wa muziki kisawasawa ni Profesa J,ambaye aliangusha vibao vyake vikali
vinavyoendelea kutamba katika soko la muziki ndani na Nje ya nchi baadhi ya
vibao vyake vikali vilivyowapagawisha mashabiki wake ni Zali la mentali wimbo
huo aliemshirikisha Sir Nature,Kamiligado,ndiyo mzee na kumalizia na kibao cha
hapo vipi ambacho kilipelekea mashabiki wake kulipuka na kuomuomba asishuke
jukwaani aendelee kutoa burudani.
Aliposhuka jukwaani mwanamuziki Mheshimiwa Temba&Chege walipanda
na kundi lake ambapo walikamua kisawasawa na kumwaga burudani iliyowafanya wapenzi
wa muziki kucheza kwa furaha na kutamani asishuke jukwaani.
Aliyefunga pazia la kutoa burudani Mtoto wa kitanga Roma Mkatoliki
naye alipagawisha wapenzi vilivyo kwa vibao vyake
mbalimbali vikiwemo vipya na vya zamani.
Hadi mwisho wa tamasha wapenzi wengi walikuwa bado wanatamani
lisiishe na baadhi yao walipohojiwa waliishukuru Vodacom Tanzania kwa kuwaandalia
wateja wao tamasha hilo la burudani kemkem,Alisema Ramadhani Malenge mkazi wa
Kawe jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu alisema
kuwa Vodacom imeamua kuwaandalia wateja wake na wakazi wa jiji la Dar es Salaam
tamasha hilo kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake
na wananchi kwa ujumla katika sikukuu ya mwaka mpya, vilevile
wananchi walipata fursa ya kujinunulia bidhaa mbalimbali za Mawasiliano
kwa gharama nafuu.
“Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “Ukiwa na Vodacom maisha ni
murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua kuwa
kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani hivyo ndio maana tunaandaa na
kudhamini matamasha ya aina hii na tutaendelea kufanya hivyo siku zote
ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga
mkono”Alisema.
Alisema mwaka huu burudani kupitia matamasha haya imekuwa jijini
Dar es salaam wakati mikakati inafanyika kuhakikisha burudani hii
inasambazwa kwa wateja wote nchi nzima “Tunawajali na kuwasikiliza wateja wetu
ambao kwetu ni wafalme hivyo tutahakikisha huduma bora na burudani katika
kipindi maalum kama hiki inawafikia katika siku za usoni”. Alisema Nkurlu.
No comments:
Post a Comment