TANGAZO


Sunday, January 4, 2015

Simba yaitafuna Mafunzo Kombe la Mapinduzi, yaifunga bao 1-0

Kocha Mkuu wa Simba, Goran akiwa na Msaidizi wake, Suleiman Matola wakijadili jambo wakati wakisubiri mpambano wa timu yao na Mafunzo, Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar jana jioni. Katika mchezo huo, Simba ilishinda bao 1-0. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews Blog)
Kocha Mkuu wa Simba. Goran akitowa maelekezo kwa mchezaji wake wakati wakifanya mazoezi mepesi mepesi kusubiri mchezo kati ya timu yao na Mafunzo uliofanyika uwanja wa Amaan.
Wachezaji wa timu ya Mafunzo wakisalimiana na wachezaji wa Simba kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Mafunzo kilichopambana na timu ya Simba na kukubali kipigo cha bao 1-0.
Kikosi cha timu ya Simba kilichoipa kipigo timu ya Mafunzo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar jana.
Mchezaji wa timu ya Mafunzo akimpita beki wa timu ya Simba wakati wa mchezo wao wa kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar. Simba ilishinda kwa bao 1-0.
 Kizazaa golini kwa timu ya Mafunzo.
Mshambuliaji wa Simba akimpita beki wa timu ya Mafunzo na kupiga krosi lakini haikuzaa matunda.
Jopo la Ufundi la timu ya Simba likiongozwa na Kocha wake Mkuu Goran, wakifuatilia mchezo kati ya timu hiyo na Mafunzo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayofanyika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Simba, Elias Maguri, akimpita beki wa timu ya Mafunzo katika mchezo wa kuwania Kombe la Mapinduzi zinazofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mshambuliaji wa timu ya Simba kutoka Uganda, Sserunkuma akiwa na mpira akimpita beki wa timu ya Mafunzo. Katika mchezo huo, Simba imeshinda bao 1-0. 
Mshambuliaji wa timu ya Simba, Elias Maguri, akiwapita mabeki wa timu ya Mafunzo.



Dan Sserunkuma wa Simba akiudhibiti mpira.
Dan Sserunkuma wa Simba akikatwa kwa nyuma na mchezaji wa Mafunzo.


Makocha wa Yanga wakiwa Uwanja wa Aman wakifuatilia mchezo kati ya Simba na Mafunzo.

No comments:

Post a Comment