TANGAZO


Saturday, January 3, 2015

Ridhiwani Kikwete aanza ziara ya kikazi katika Vijiji 40 vya Jimbo lake la Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali ya Vijijini kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobomoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo. Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda)
Ridhiwani Kikwete akikagua Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobomoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni
Moja ya jengo la Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani iliyoezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.  
Ridhiwani Kikwete, akitoa mipira kwa vijana.
Watioto wakiruka mtaro kumuwahi Ridhiwani Kikwete alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu.
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Watoto wakigawiwa ndizi na Ridhiwani. 
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja ambapo aliwaahidi kutatua tatizo la mawasiliano ya simu kwa kuwapelekea mnara. 
Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja.
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma, Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi  kuboresha barabara na mawasiliano ya simu.
Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika Kijiji cha Kwa Mduma wakati wa ziara yake katika jimbo lake la Chalinze, Kata ya Kibindu.

No comments:

Post a Comment