Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakikata utepe kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar(kushoto0 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakifungua pazia kwa pamoja kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Wananchi na Viongozi mbali mbali walioalikwa katika sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Ndege zmbali mbali zikiwa katika Paki ikionesha sura halisi ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar ilivyo ambapo Ndege za mashirika mbali mbali ya ndege zinaouwezo wa kutua hapa nchini na kuweza kukuza pato la Taifa letu.
Msoma Risala Farida Rajab Yussuf akisoma risala hiyo mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Wasanii wa Ngoma ya Kibati wakitoa burudani yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) uzinduzi uliofanyika leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alikuwa mgeni rasmi wa shuhuli hiyo.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akitoa nasaha fupi na kumkaribishaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezitaka taasisi za serikali na binafsi
zinazofanya kazi katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuacha
mivutano na badala yake washirikiane ili kuufanya uwanja huo kuwa ni kichocheo
katika kukuza biashara na kuimarisha sekta ya utalii hapa nchini.
Dk. Shein
aliyasema hayo leo huko Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar mara baada ya
kuzindua maegesho na njia ya kupitia ndege katika kiwanja cha Kimataifa cha
Abeid Amani Karume Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 51 ya
Mapinduzi ya Zanzibar ambapo viongozi mbali mbali na wananchi walihudhuria
akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd.
Katika maelezo
yake Dk. Shein alisisitiza kuwa taasisi hizo ni lazima zikae pamoja na
kushirikiana katika mambo na maamuzi yao kuamua wenyewe na si kupeleka
Serikalini huku akiwataka kuanza taratibu hizo mapema kabla ya ujenzi wa jengo
jipya la abiria hivi karibuni.
Aidha, Dk. Shein
aliwataka watendaji na viongozi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na
Serikali katika uwanja huo ikiwa ni pamoja na matumizi ya VIP na kuwataka
viongozi kufuata sheria ya Mamlaka ya viwanja vya ndege iliyowekwa.
Alisema kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo tayari ameshapewa taratibu zote na tayari
sheria ipo ambayo imepitishwa katika Baraza la Mapinduzi na kushangazwa na
viongozi wanaowasakama wafanyakazi wa uwanja huo kwa kutofuata sheria na
taratibu ziliopo.
“Tusirudishe
nyuma taratibu zilizowekwa na Serikali katika uwanja wetu huu wa ndege na kila
kiongozi anawajibu wa kufuata taratibu na sheria zilizopo sisi sote nadhani
tunasafiri tunaenda Kusini, Kaskazini, Mashariki na Magharibi tunaona katika
viwanja vya wenzetu wanavyokuwa makini... iweje sisi tuwe hivi”,alisema Dk.
Shein kwa mshangao mkubwa.
Dk. Shein pia,
alisisitiza kuwa suala la ulinzi na usalama ni la lazima katika viwanja vya
ndege hivyo, ni lazima kuwepo ulizni wa uhakika katika uwanja huo ili kufuata
sheria na taratibu za kimataifa za viwanja vya ndege ikiwa ni pamoja na kuwepo
kwa huduama za zimamoto za uhakika.
Pia, Dk. Shein alieleza azma ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kukijenga kiwanja cha ndege cha Pemba ndani ya mwaka huu ikiwa
ni pamoja na kukiweka taa ili ndege ziweze kutua na kuruka wakati wa usiku ili
uwanja huo uwe na hadhi inayokubalika.
Alisema kuwa tayari
wameshajitokeza washirika wa maendeleo kutoka nchini Uturuki ambao wameonesha
nia ya kukijenga kiwanja hicho cha ndege cha Pemba. Aidha, alieleza azma ya
Serikali ya kujenga gati kubwa huko Mkoa wa Kaskazini Pemba ili kuepuka
usumbufu wanaoupata wananchi wa Mkoa huo kwenda mkoa mwengine wa Kusini kufuata
huduma hiyo.
Katika hotuba
yake hiyo Dk. Shein alisikitishwa na kutokuwepo kwa takwimu za uhakika za
uingiaji wageni katika uwanja huo wa ndege na kushangazwa na mamlaka zilizopo
katika kiwanja hicho kwa kuchelea kutoa takwimu sahihi hali ambayo alisema
inapelekea kuzorota kwa maendeleo hasa katika sekta ya utalii ambayo ndio nguzo
kubwa ya uchumi wa Zanzibar.
Alionesha
kushangazwa huko kwa kuwa utaratibu tayari umeshawekwa na kuzitaka taasisi
zilizomo ndani ya uwanja huo kushirikiana kwa pamoja na kuacha mivutano kwani
mivutano haijengi na badala yake inabomoa.
Alisema kuwa
licha ya uhaba wa eneo liliopo ndani ya uwanja huo lakini haja ya kufanya kazi
kwa kushirikiana ni muhimu kwani serikali baada ya kuliona tatizo hilo la uhaba
wa eneo ndipo ilipolazimika kujenga jengo jipya la abiria.
Dk. Shein
alisisitiza haja ya kuyaita mashirika ya ndege kuzileta ndege zao hapa Zanzibar
kutokana na upanuzi huo wa uwanja wa ndege ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa
jengo jipya la abiria katika kiwanja hicho cha ndege cha Abeid Amani Karume
Alisema kuwa
lengo kubwa ni kuirejesha Zanzibar kuwa kituo kikubwa cha kibiashara kama
ilivyokuwa hapo siku za nyuma mnamo karne ya 19 na 20 ambapo Zanzibar iliweza
kufanya biashara na Hongkong, Machester na sehemu nyenginezo.
Alisisitiza kuwa
mbali ya malengo na jitihada hizo, pia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ndani ya
mwaka huu inakusudia kuingiza watalii laki5 kwani ujenzi wa huduma hizo za
kiwanja cha ndege ni miongoni mwa vichocheo vikuu vya maendeleo.
Dk. Shein pia
amezitaka taaisi zinazofanya kazi ndani ya uwanja huo wa ndege wa Kimataifa wa
Zanzibar ziweze kubuni mambo mbali mbali na kuwa chanzo cha kushajiisha
maendeleo yao katika uwanja huo.
Aidha, Dk. Shein
aliipongeza Kamati ya watu saba iliyokuwa ikiongozwa na Marehemu mzee Juma Ame
ambayo imefanya kazi kubwa katika kuwatuliza wananchi wa eneo hilo la uwanja wa
ndege baada ya kutokea mtafaruku mkubwa wakati wa ujenai huo ambapo wananchi
hao walitakiwa nyumba zao kuvunjwa.
Naye Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Juma Duni Haji alisema kuwa mafanikio makubwa
yameweza kupatikana katika ujenzi huo na kueleza azma ya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar katika ujenzi huo.
Aidha, Waziri
huyo alitumia fursa hiyo kueleza changamoto zilizopo na juhudi za ufumbuzi
zinazochukuliwa huku akieleza kuwa
tayari mashirika makubwa yameshaanza safari zake hapa Zanzibar na kueleza
matarajio ya mashirika mengine makubwa duniani yakiwemo Qatar, Emirate, Fly
Dubai, Turkish na mengineyo.
Mwakilishi wa
Benki ya Dunia, Monthe Biyoundi nae alieleza kufarajika na hatua hiyo ya ujenzi
iliyokamilika katika uwanja huo wa ndege wa Zanzibar na kusisitiza azma ya
Benki hiyo ya kuendelea kuiunga mkono Zanzibar.
Mapema Katibu
Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk. Juma Malick Wakili akitoa
maelezo ya kitaalamu alisema kuwa mkataba wa ujenzi huo ulitiwa saini baina ya
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na Kampuni ya SOGEA SATOM ya Ufaransa
mnamo tarehe 18 Mei 2012 kwa gharama za Tsh. Bilioni 65.6.
Alisema kuwa
mradi huo ulitarajiwa kuanza rasmi tarehe 02Julai 2012 baada ya utiaji saini,
lakini kutokana na sababu mbali mbali za kiufundi mkandarasi alianza ujenzi
Novemba 29, 2012 na kukamilika rasmi baada ya siku 740 yaani tarehe Disemba 9,
2014.
Alisema kuwa
baada ya kukamilika kwa Mradi huo Kiwanja hicho kitakuwa na njia sita za
kupitia ndege kuelekea na kutoka katika barabara ya kurukia na kutulia ndege
zenye urefu wa mita 3,427 na upana wa mita 25 na mabega yenye upanda wa mita
9.5 kila upande.
Sambamba na hayo,
Katibu Mkuu hyo alisema kuwa Serikali ya Mapindyuzi Zanzibar ilitumia jumla ya
Tsh. Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi waliokua wakitumia eneo
la mradi kama makaazi na amshamba yao pamoja na fidia ya kuhamisha makaburi 21
yaliokuwemo katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment