Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali
Mohamed Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi
(katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Kadhi Mkuu wa
zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) Waziri wa katiba na Sheria Abubakar
Khamis Bakary akifuataiwa na makamo wa Pili wa Rais Alhaj Seif Ali Iddi
wakisimaa kwa pamoja na waislamu wengine na Viongozi wakati wa Kumswalia
Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) katika sherehe ya Maulid iliyofanyika jana
viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja.(Picha zote na
Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali
Mohamed Shein (kulia) wakati alipojumuika na Mashekhe, Viongozi na
Waislamu mbali mbali katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana
Mtume Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara
Suleiman Mjini Unguja,(pichani) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar
Kabi akitia ubani kama ishara ya Ufunguzi wa Maulid hayo.
Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakia
Bilali (katikati) akiwa na Wake wa makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar
Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) na Mama Pili balozi Seif (kulia)
pamoja na Wake wa Viongozi mbali mbali na wananchi wa kawaida
wakijumuika katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume
Muhmmad S.A.W
yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja
ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguo sita.
Akina Mama kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na Vitongoji vyake
wakiwa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja palipofanyika
sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W ambapo
hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita na mgeni rasmi
alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.
Ali Mohamed Shein.
Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali vya Quran na Waislamu mbali mbali
waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad
S.A.W zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini
Unguja kama wanavyoonekanwa Pichani.
Wanafunzi wa Madrasatul Dhuriyatul Islamia kutoka Kisiwani Tumbatu Mkoa
wa Kaskazini Unguja wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid
Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana
katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali
Mohamed Shein.
Ustadh salum Rashid kutoka Amani Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Mlango
wa Barzanji(4) wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana
Mtume Muhammad (S.A.W.)
zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele
ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
No comments:
Post a Comment