TANGAZO


Sunday, January 4, 2015

Maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) Dar es Salaam

Mgeni rasmi katika maadhimisho Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Sheikh Mkuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, akitoa salamu za Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), wakati wa maadhimisho hayo.
Waumini wa Kiislamu, wakiongozwa na Sheikh Mkuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, katika dhikri wakati wa kusomwa mlago wa 6 wa maulid hayo.
Waumini wakiwa katika kisimamo cha kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), viwanjani hapo. Wapili kulia ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu.
Kadhi Mkuu wa Tanzania,  Sheikh Abdallah Mnyasi (kushoto), akisoma dua ya kufunga maadhimisho hayo, huku mgeni rasmi Abdulrahman Kinana (wapili), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Ramadhan Madabida, wakishiriki dua hiyo. 
Kadhi Mkuu wa Tanzania,  Sheikh Abdallah Mnyasi (kushoto), akiwa na mgeni rasmi Abdulrahman Kinana (wapili), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Ramadhan Madabida katika maadhimisho hayo. 
Waumini wakiwa katika kisimamo cha kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), viwanjani hapo.
Akinamama wakiwa katika maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Ustaadhi akighani maulid katika mlango wa 3.
Mtoto akiwa na baba yake akimtunza msomaji wa Maulid.

No comments:

Post a Comment