TANGAZO


Thursday, January 1, 2015

Pulis ndiye kocha mpya wa Westbromwich

Meneja mpya wa kilabu ya West Bromwich Tony Pulis
Tony Pulis ndiye kocha mpya wa kilabu ya West Bromwich na atahudumu kwa kandarasi ya miaka miwili na nusu ,kilabu hiyo imetangaza.
Pulis ataanza kazi baada ya mechi ya Alhamisi ugenini West Ham huku mechi yake ya kwanza ikiwa ile ya kombe la FA dhidi ya Gateshead.
Katika kile kilichoonekana kama ushindani kati ya Pulis na Tim Sherwood baada ya kufutwa kazi kwa kocha Alan Irvin,bodi ya Westbrom iliamua kuwa Pulis ambaye alitajwa kuwa meneja bora wa ligi ya EPL mwaka huu baada ya kuiimarisha kilabu ya Crystal Palace msimu uliopita alikuwa kocha bora.

No comments:

Post a Comment