TANGAZO


Monday, January 5, 2015

Mourinho aomba radhi kumkosoa mwamuzi

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho
Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amemuomba radhi mwamuzi Kevin Friend baada ya kumkosoa kwa kuwanyima penati katika mchezo wa Kombe la FA ambao walishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Watford jana.
Mourinho alidai kuwa uamuzi wa kunyimwa penati baada ya Craig Cathcart kushika mpira uliopigwa na Diego Costa kuwa ni sehemu ya kampeni za kuikandamiza timu yake.
Lakini baadae Mourinho alibadili kauli yake na kumpongeza mwamuzi huyo kwa kuchezesha vyema.
Mwamuzi huyo alifafanua uamuzi wake kuwa aliwanyima penati Chelsea kwani mshambuliaji huyo alifunga bao pamoja na mpira kushikwa na kama ingetokea bao kutofungwa angekuwa hana jinsi bali kutoa penati.

No comments:

Post a Comment