Siku
ya choo duniani ambayo huadhimishwa tarehe 19 Novemba. UNIC
waliadhimisha siku hii kwa kuwakutanisha vijana walioko nje ya shule
tarehe 23 Desemba 2014 kwa lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha
utumiaji wa vyoo ili na wao waweze kuelimisha jamii zinazowazunguka juu
ya umuhimu wa kuwa na vyoo.
Tukio
hili liliwakutanisha vijana toka vikundi 5: Azimio Youth Group,
Makangarawe Youth Development Fund, Mashine Ya Maji Youth Development
Centre,Temneke Youth Development Foundation na Tanzania Youth
Development Society. Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha.
Vijana wakiwa katika makundi kujadili na kuweka mikakati watakavyosaidia jamii kuhusu utumiaji wa vyoo na usafi wa mazingira.
Afisa
Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi.Usia
Nkhoma-Ledama akitoa mada kuhusu siku ya Choo duniani pamoja na umuhimu
wa utumiaji vyoo, na kampeni maalumu ya uhamasishaji wa kuwa na vyoo.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Asasi za Vijana Temeke (Temeke Youth Development Network
-TEYODEN), Ismail Mnikite akitambulisha vijana waliohudhuria kutoka
makundi mbalimbali.
Baada
ya majadiliano, vijana wakiwasilisha maazimio na
mikakati waliyoyakusudia kufanya ndani ya vikundi vyao katika jamii
zinazowaunguka.
No comments:
Post a Comment