TANGAZO


Wednesday, December 24, 2014

Mkandarasi Geofrey Mungai atoa msaada wa zaidi ya sh. milioni 2 kwa yatima kwa ajili ya Krismas DBL

Sarah  Mungai  akisoma risala  ya  familia  ya mkandarasi Geofrey  Mungai kusaidia yatima  misaada  yenye thamani ya  zaidi ya Tsh  milioni 2 kwa  ajili ya kufanikisha watoto hao wa  kituo  cha Daily Bread  Life Childreans home kusherekea  sikukuu ya krismas kwa furaha  zaidi (Picha na Francis Godwin)

Na Francis Godwin, Iringa
MKANDARASI  Geofrey  Mungai  ametoa  msaada  wa  nguo za sikukuu na chakula vyote  vikiwa na  thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2  kwa kituo cha  watoto yatima cha  Daily Bread Life Tanzania  (DBL) kwa ajili ya  kusherekea sikukuu ya krismass na mwaka mpya.
Mungai alitoa  msaada huo jana,  kwa  uongozi  wa  kituo hicho pamoja na kuwaandalia chakula  cha pamoja   watoto  zaidi   39  na  wananchi mbali mbali wa mji  wa Iringa kama njia ya  kuwahamasisha  kusaidia yatima .

Akizungumza  kwa niaba ya familia ya Mungai mke wa mkandarasi huyo Sarah Mungai   alisema  kuwa imekuwa ni kawaida  yake  kwa  kila mwaka katika msimu  wa  sikukuu ya Krismas na mwaka  mpya  kufika katika  kituo hicho na  kuwapa msaada  watoto  hao  ili nao  kuungana na  watoto  wenye  wazazi  wao kufurahia sikukuu hizo.
Hata  hivyo  alisema  kuwa jamii ya  mkoa  wa Iringa na  watanzania  kwa ujumla wanapaswa  kubadilika kwa  kuelekeza  michango  yao  kwa  watoto  yatima ambao baada ya  kupoteza  wazazi  wao  faraja ya  pekee  wanaisubiri  kutoka kwa  jamii inayowazunguka.
Aidha  alisema  kuwa  yeye  kama mmoja kati  ya wananchi wa Iringa wenye mapenzi mema na watoto yatima hivyo kuwaomba wananchi wengine   kuweka  mpango wa  kuendelea  kutembelea  vituo  vya yatima kila mwaka  kwa  ajili  ya kuwasaidia misaada  mbali mbali.
Alisema  kuwa  upo uwezekano mkubwa wa  watoto  hao yatima  kuendelea   kusaidia  iwapo watanzania na wadau  mbali mbali   kuwekeza kwa  watoto hao.
Kwa  upande  wake  mkurugenzi mtendaji  wa  kituo  hicho  mchungaji Mpeli Mwaisumbi mbali ya  kumpongeza  Mungai kwa  kuendelea  kusaidia  watoto  hao  bado wadau  mbali mbali  wameendelea kujitolea kusaidia  kituo hicho .

"watoto  hao wanalilewa  vema na  wapo ambao  wanasoma shule  mbali mbali   na  vyuo  vikuu baada ya kusaidiwa na  wadau"

 Alisema  kuwa  kituo  hicho kinafanya kazi  chini  ya  shirika  lisilo la kiserikali  ya Daily Bread  Life  Tanzania lililosajiliwa  kwa  usajili  12903 chini ya  wizara ya mambo ya ndani ya  nchi pia   kituo  kimesajiliwa na ustawi  wa jamii kwa  kupewa usajili wa Makao  ya  watoto namba 00049995.
Hata  hivyo  alisema  kuwa  kituo  kilianza  kupokea  watoto  14 mwaka  2004 na  sasa  kuna  watoto 37 waliopo  kituoni  hapo  na  kuwa  toka  kituo  kianzishwe  jumla  ya  watoto 51 wamelelewa  hapo.
Alisema  kutokana na misaada wa  wadau mbali mbali kituo kimeendelea  kupata  mafanikio makubwa kama  kuwa na  shamba  ,basi  moja ,mradi  wa cherehani pia  tayari   shule  ya  sekondari ya DBL imejengwa na imeanza  kupokea wanafunzi toka mwaka huu  shule  iliyopo  umbali  wa kilomita 6  kutoka mjini Iringa kwa  lengo kuwawezesha  watoto  na wengine  watyakaofaulu na kukosa nafasi  kupata  elimu ya  sekondari.
Pia  alisema changamoto  kubwa katika  uendeshaji wa  kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi ambako  watoto  hao  wanasoma ,kukosa  ruzuku toka  serikalini na  changamoto  nyingine  nyingi.
Mchungaji Mpeli  aliwaomba  watanzania  na  wadau mbali mbali pale  walipo  iwapo  wanahitaji kusaidia  kituo hicho  kutuma  michango  yao kupitia akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007  Daily Bread  Life Childreans home ,ama  kwa njia ya M-PESA  0754362536

No comments:

Post a Comment