TANGAZO


Wednesday, December 24, 2014

Kizigha atembelea Wajumbe wa Jumiya ya Wazazi Ilala, Temeke na Kinondoni kuwashukuru

 Katibu Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Chollaje Ally, akizungumza na wajumbe wa Jumuiya hiyo, Jimbo la Tameke, wakati Mwenyekiti wa Jumiya hiyo, mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha alipofanya ziara jimboni humo jana.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Katibu Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Chollaje Ally, akizungumza na wajumbe wa Jumuiya hiyo, Jimbo la Tameke, wakati Mwenyekiti wa Jumiya hiyo, mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha alipofanya ziara jimboni humo jana.
 MBUNGE wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam (CCM), Angela Kizigha akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi, alipofika Temeke kuwashukuru na kuwapa zawadi ya Krismasi na Mwaka mpya wajumbe hao jana. 
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam (CCM), Angela Kizigha akizungumza na wajumbe wa Jumuiya hiyo, Jimbo la Temeke.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam (CCM), Angela Kizigha akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi, wakati alipokutana nao jana.
 Katibu Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Chollaje Ally, akizungumza na wajumbe wa Jumuiya hiyo, Jimbo la Kinondoni, wakati Mwenyekiti wa Jumiya hiyo, mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha alipofanya ziara jimboni humo jana.
Katibu Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Chollaje Ally, akizungumza na wajumbe wa Jumuiya hiyo, Jimbo la Kinondoni, wakati Mwenyekiti wa Jumiya hiyo, mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha alipofanya ziara jimboni humo jana.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam (CCM), Angela Kizigha akimvisha khanga mmoja wa wajumbe wa jumuiya hiyo, wakati wa ziara yake hiyo jana. 

Na Charity James
MBUNGE wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam (CCM), Angela Kizigha ametoa pongezi za dhati kwa Rais Kikwete kutokana na uamuzi alioutoa alipokutana na wazee wa Dar es Salaam.
Rais amekisafisha chama kutokana na baadhi ya watu wachache walio jihusisha na uchotaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, kuwataka watanzania kuacha kukihukumu chama kutokana na watu wachache.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana wakati akikabidhi zawadi kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo alitoa kwanga kwa wajumbe wote waliohudhulia mkutano pamoja na zawadi za sabuni, Pampasi kwaajili ya wazazi katika hospitali za Temeke, Ilala na Kinondoni.

"Unajua krisimasi kwa sisi wakristo tunasema ni siku ya kuzaliwa yesu kristo na waisramu wanasema kuzaliwa kwa nabii Issa hivyo tunapenda kutumia nafasi hiyo kutoa zawadi katika wodi za wazazi," alisema.
Kizigha alitumia nafasi kwa kusema kuwa viongozi wowote watakaobainika kukisaliti chama kipiti cha uchaguzi wa serikali za mitaa watasimamishwa na kufutwa uongozi kabisa.

"Katika tukio la wanachama waliosaliti chama watachunguzwa na endapo watadhibitika kusaliti watachukuliwa hatua, tutahakikisha mtu anachukuliwa hatua kwa kuthibitisha ili kukwepa watu tuchukuliwa hatua kutokana tofauti za kisiasa," alisema.

Naye Katibu Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Chollaje Ally alisema umefika wakati wa kuchagu viongozi na sio kuchagua safu.
Pia aliwataka wajumbe wote waliochagua viongozi na kuhamasisha wanapiga kampeni za kuhamasisha wananchi kuchagua CCM kuyaweka wazi matatizo yaliyojitokeza katika chaguzi kuwekwa wazi ili yaweze kutatuliwa.

Alisema kwa kufanya hivyo wanaamini katika chaguzi zijazo ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa madiwani wanashinda kwa kishindo.

No comments:

Post a Comment