Tanzania imechaguliwa na shirikisho la mpira wa wavu Afrika (CAVB) kuwa wenyeji wa michuano ya kanda ya Tano ya Beach Volleyball ( mpira wa wavu ufukweni).
Michuano hiyo itakayofanyika kuanzia February 16-18 mwakani itakuwa ni sehemu ya kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2016.
Mkurugenzi wa Kamisheni ya wavu ufukweni, Muharrami Mchume amesema wapo tayari kwa uwenyeji na kuongeza kuwa Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti na wenyeji Tanzania ndio nchi zitakazoshiriki.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Mchezo wa mpira wa wavu sio maarufu sana nchini Tanzania licha ya kuwa na fukwe nyingi za bahari.
CAVB ipo katika jitihada za kuendeleza mchezo huo wa ufukweni na hivi karibuni liliendesha semina nchini Tanzania ambayo ilishirikisha washiriki kutoka zaidi ya nchi tano katika jitihada za kuukuza mchezo huo katika nchi za kanda ya tano hasa mashuleni.
Michuano hiyo inategemewa kufanyika katika fukwe za beach ya Mbalamwezi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment