TANGAZO


Wednesday, December 31, 2014

Serikali yatakiwa kusitisha uporomokaji wa bei za Filamu Nchini

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel aliyesimama akifungua Mkutano  Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini  (hawapo pichani)kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu, wa pili kutoka  kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini. Bi. Joyce Fissoo.Mkutano huo ulifanyika  jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo aliyasimama akifafanua jambo kwa wadau wa usambazaji wa Filamu nchini wakati wa Mkutano wa Baina yao na  Serikali uliofanyika jijini Dar es Salaam,wakwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mwanasheria wa Wizara Bw. Patrick Kipangula.
Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel (hayupo pichani) akifungua Mkutano wa wasambazaji wa Filamu nchini kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.(Picha zota na Benjamin Sawe)

Na Genofeva Matemu – Maelezo
Tarehe: 31/12/2014
SERIKALI imewapongeza wasambazaji na wadau wa filamu nchini kwa mchango wao mkubwa katika kuelimisha, kuhabarisha na kufundisha maadili ya Mtanzania huku wakichangia katika pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua mkutano wa Serikali na wasambazaji wa filamu nchini jana jijini Dar es Salaam kujadili uporomokaji wa bidhaa za filamu nchini.

“Tunathamini sana kazi mnayoifanya, Serikali inawajali na ipo tayari kushirikiana nanyi kwa kazi nzuri mnayoifanya hivyo ni vema kufanya mkutano huu kuwa wa kisanyansi kwa kuangalia gharama mnazotumia kuandaa bidhaa za filamu ili kuweza kukua kibiashara na kukuza uchumi wa nchi” amesema Pro. Gabriel.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo amesema kuwa Bodi haitaruhusu bidhaa zilizo chini ya kiwango kupelekwa kwa Watanzania kwa daraja la bei ya chini pamoja na soko huria kwani hakuna uhuria usio na mipaka.

Bibi Fisoo amesema kuwa wananchi siyo dust bin wanapaswa kupelekewa kazi bora na zenye hadhi kwani Bodi inahitaji kujiridhisha kuhusu viwango vya filamu hizo na kuheshimu fedha za watanzania kwa kuwauzia kazi bora zinazoendana na thamani ya fedha zao.

Aidha Mwenyekiti wa wasambazaji wa bidhaa za filamu nchini Bw. Emmanuel Miamba amewataka wadau na wasambazaji wa filamu nchini kuwa wakweli, wazalendo, pasipo kuogopa kitu chochote na kuangalia maslai ya wasambazaji wote na kama wataona uwekezaji katika kazi za filamu haulipi basi wawekeze katika masuala mengine na sio kushusha bei kuua tasnia ya filamu nchini.


Naye Bw. Chacha Matula kutoka Jembe Entertainment amewaomba wasambazaji kuwa na umoja na mshikamano utakaowawezesha kushirikiana kwa pamoja na serikali kusitisha uporomokaji wa bei za filamu na kuwadhibiti watu wanaotaka kuua kampuni za wasambazaji wadogo nchini.

No comments:

Post a Comment