Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa
wa Mbeya Mkunde Said (kushoto), akimpima
kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Fikiri Sabigo kwa
kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa
kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait to
Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi
wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom Tanzania
kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja Zoezi hili lilifanyika leo katika
kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani katika mwendelezo wa
kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Dereva wa mabasi yaendayo mikoani Mohamed Shaban(kushoto)akipimwa
kiwango cha pombe mwilini na Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama
Barabarani mkoa wa Mbeya,Mapunda Ahmed(kulia)kwa kutumia kifaa maalum wakati wa
upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama
Barabarani ya”Wait to Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto
kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni
Nashon Mudala mtaalam wa usalama na Afya na mazingira wa Vodacom Tanzania.Zoezi
hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya yaendayo
mikoani katika mwendelezo wa kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na
kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani
mkoa wa Mbeya Mapunda Ahmed (kulia)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa
basi la kwenda mikoani, Simon Mwalugu kwa kutumia kifaa maalum wakati wa
upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama
Barabarani ya”Wait to Send” unaohamasisha
madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa
wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda
za juu kusini Macfadyne Minja.Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha
mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni hiyo
inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini
Macfadyne Minja(katikati)akimfafanulia jambo kuhusiana na kampeni ya “Wait to
Send”dereva wa basi la kwenda mikoani, Simon Mwalugu.Wakati wa zoezi la upimaji
wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani zoezi hilo
lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo
wa kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom
Tanzania,kulia . Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa
wa Mbeya Mapunda Ahmed.
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani
mkoa wa Mbeya Mkunde Said
(kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda
mikoani, Emanuel Mkulangya kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva
ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait to Send” unaohamasisha madereva wa
vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo
hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini
Macfadyne Minja Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani
Mbeya yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni hiyo inayofanyika nchi
nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Jeshi la Polisi-Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa
wa Mbeya Butusyo Mwambelo katikati akimwelezea jambo dereva wa mabasi yaendayo
mikoani Julius Mkasanga(kulia)wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe
mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani zoezi hilo lilifanyika leo
katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo
inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,wapili kushoto ni
Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja.
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani
mkoa wa Mbeya Mapunda Ahmed (kulia) akihakiki leseni ya dereva wa mabasi
yaendayo mikoani Simon Mwalugu(kushoto)wakati wa zoezi la kupima kiwango cha
pombe mwilini kwa madereva wa mabasi ya kwenda mikoani, kwa kutumia kifaa
maalum ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait
to Send” unayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za
mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom
Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja.Zoezi hili lilifanyika
leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya.
Na Mwandishi wetu, Mbeya
Na Mwandishi wetu, Mbeya
KAMPENI ya usalama
barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani
iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe,leo
imeendelea mjini Mbeya.
Madereva wameendelea
kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au
kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya
moto.
Mkuu wa kikosi
cha usalama barabarani wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Butusyo Mwambelo
amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa
barabara hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia
maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo
mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema.
Alisema madereva
wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea
kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu
ya Krismas na mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono
jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu.
Kwa upande wake,Mkuu wa kanda
ya Nyanda za juu wa Vodacom Tanzania Macfadyne Minja, alisema Vodacom
itaendelea kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za
kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili
kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunaomba madereva kufuata
sheria za barabarani kwa usalama wenu,usalama wa abiria mnaowabeba na
watumiaji wengine wa barabara".
Aliongeza kuwa
Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari
wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya
"Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria
za usalama barabarani.Mbali na kampeni hii alisema kwa mwaka huu kampuni
ilidhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
Alisema kabla ya
uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa madereva
kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na
kampeni itaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.
Katika kampeni ya leo
wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa usalama barabarani
na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabani walitoa uhamasishaji
kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia
madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi
wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini
kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendeshwa
vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment