Klabu ya Yanga Tanzania imesema ina inamatumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya soka kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kupangwa dhidi ya Timu ya BDF ya Botswana katika Raundi ya awali ya michuano hiyo .
Katika michuano hiyo ya soka kombe la shirikisho Yanga ya Dar es salaam itaanzia nyumbani katika mechi ya awali dhidi ya klabu ya BDF ya Botswana na endapo itasonga mbele itakutana na mshindi katika ya sofapaka ya Kenya na platinum ya Zimbabwe .
Afisa Masoko wa klabu ya Yanga OMARY KAYA ameelezea matumaini Timu yake kuhusu mechi hiyo amesema watafanya vizuri kufuatia maandalizi watakayofanya kuelekea mchezo huo kwa kuwa bado timu ina nafasi kubwa ya kufanya maandalizi ya kutosha .
Katika michuano hiyo ya afrika kwa upande wa vilabu ,mabingwa wa soka Tanzania bara Azam FC wataanza Nyumbani na El Merrikh ya Sudan katika ligi ya mabingwa ya soka baarani afrika , huku KMKM, ya Zanzibar wakicheza Ugenini dhidi Hilal ya Sudan , wakati Polisi ya Zanzibar itaanza Ugenini na CF Mounana ya Gabon katika kombe la shirikisho.
No comments:
Post a Comment