TANGAZO


Wednesday, December 31, 2014

Dk. Pindi Chana: Kila mtoto ana haki ya kupendwa, kulindwa na kuheshimiwa

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akuzngumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Haki na Ulinzi wa mtoto. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Haki na Ulinzi wa mtoto. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Vickness Mayao na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Haki na Ulinzi wa mtoto. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Missani na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akifafanua jambo katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.
Waandishi wa habari, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.
 Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Haki na Ulinzi wa mtoto. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Missani na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Haki na Ulinzi wa mtoto. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Missani na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake, Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Judy Kizengo.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Missani, akijibu maswali ya waandishi wa habari. Kulia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Vickness Mayao, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana.

Na Edith Msuya

SERIKALI imesema haitowavumilia na kwamba itawachukulia hatua wale wote wanaokwenda kinyume na haki za msingi za watoto wa kike au wakiume wanaobaguliwa na wazazi, walezi au jamii.
Pia, imesema haitakubali ubaguzi wowote unaotokana na hali yake ya kimaisha kama vile utajiri au umaskini, uadilifu ugonjwa ulemavu na jinsi anavyoonekana mbele za watu.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia  na Watoto Dk, Pindi Chana alisema kila mtoto ana haki ya kupendwa na kuheshimiwa kulindwa na kutobaguliwa.


Chana alisema kwa sasa kuna kamati 25 zilizoundwa kwa ajili ya ulinzi wa mtoto, ambapo zinajumuisha wataalamu wa kila aina walioko wilayani.

"Serikali ili kudhibiti suala la ukatili kwa watoto, pia tuliamua kuzindua namba ya simu ambayo ni 116 mwaka 2013 ili kuwasaidia watoto kutoa taarifa za ukatili na uzalilishaji," alisema Chana.

Pia, alisema kuwa tangu ulivyoanzishwa mtandao huo walishapokea simu 24,400 zilizopigwa katika kituo cha kupokelea simu za mtandao namba 116 zikiwa na taarifa mbalimbali.

"Kati ya simu hizo nyingine zilikuwa zinahusu vitendo vya ubakaji 107, unyanyasaji wa kingono 23, usafirishaji haramu wa binadamu 21, ajira kwa watoto 47, mimba za utotoni12, ndoa za utotoni 23, kutelekeza watoto 69 na ukeketaji 11," alibainisha.
Naibu waziri huyo alisema kesi zote walizozipata tayari kwa asilimia kubwa wameshazifanyia kazi na kuwasaidia watoto wote na wale wanaotuhumiwa.

No comments:

Post a Comment