Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM akiweka jiwe la msingi la Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina, Ahmada Yahya Abdulwakil akitoa ufafanuzi wa ujenzi mbele ya Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Tawi hilo.
Mlezi wa CCM Mkoa wa Maghribi Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi mzima wa Tawi la CCM Mmobasa kwa Mchina, Wilaya ya Dimani na Mkoa wa Magharibi mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi hilo.
Wanachama wapya 79 wa CCM na Jumuiya
zake wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina wakila liapo mara baada ya
kukabidhiwa kadi na Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif Ali Iddi. (Picha zote na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ)
Na Othman Khamis Ame, OMPR
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi
alisema wimbi la vijana wa vyama vya upinzani kuamua kuvihama vyama
hivyo na kujiunga na CCM ni dalili za umadhubuti wa chama hicho
unaoonekana kuimarika kila wakati.
Alisema
chama cha Mapinduzi chenye sera na ilani imara inayokiwezesha kushinda
kila baada ya miaka mitano tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya
siasa Tanzania ndio kimbilio la watu wote wenye busara ya kutaka
kujiunga na ulingo wa siasa.
Balozi
Seif Ali Iddi ambae pia ni Mlezi wa Mkoa wa Magharibi Kichama alisema
hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la Chama cha
Mapinduzi Mombasa kwa Mchina Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi.
Alisema
makundi ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanaoamuwa wenyewe kuvihama
vyama vyao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ni muelekeo wa ishara kwa
CCM kuendelea kuongoza dola katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.
Hata
hivyo Balozi Seif aliwatahadharisha Viongozi na Wanachama wa CCM wasikae
na kubweteka na mawazo ya kushinda uchaguzi bila ya sera na mikakati ya
kujipanga vyema kwa ajili ya ushindi huo.
Aliwaomba
wana CCM popote pale walipo nchini Tanzania kuendelea kushikamana na
kuacha majungu, fitna na makundi ili ushindi uwe rahisi zaidi ya
chaguzi zote zilizopita za mfumo wa vyama vingi hapa Nchini.
Balozi
Seif aliupongeza Uongozi, wanachama na wapenzi wa chama hicho
waliojitolewa kwa nguvu zao na kuhakikisha kwamba ujenzi wa Tawi la
Mombasa kwa Mchina unasimama imara.
Alisema
licha ya kuungwa mkono na wapenzi na watu tofauti katika ujenzi wa Tawi
hilo lakini nguvu za ukamilishaji wa tawi hilo zitaendelea kubakia
mikononi mwa Viongozi pamoja na Wanachama wenyewe wa Tawi hilo.
Aliutaka
uongozi wa Mkoa wa Magharibi kuwa na tahadhari ya uvamizi wa makaazi
unaofanywa na baadhi ya watu kwa lengo maalum la kuongeza nguvu za
kuimarisha vyama vya kisiasa katika kujiandaa kwa uchaguzi Mkuu ujao.
Balozi
Seif akiwa pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwakumbusha
masheha na Wakuu wa Wilaya nchini kuendelea kufuata sheria za nchi
ipasavyo ili kila mwenye haki yake anapata fursa bila ya
vikwazo,ubaguzi wala itikadi za kisiasa.
Alisema
tabia ya baadhi ya watu zaidi wana siasa kushindikiza masheha kutoa
vibali kwa wafuasi au vijana wao kwa kutaka kupatiwa vitambulisho vya
Mzanzibari Mkaazi wakati muda wa ukaazi wa vijana hao haujatimia ni
kuvunja sheria za nchi.
“ Suala
hili la kutishwa masheha na kulaumiwa Wakuu wa Wilaya nililikemea
nilipokuwa katika ziara yangu wiki hii Kisiwani Pemba. Na hapa nalirejea
tena kwa kuwakumbusha masheha na wakuu hao wa Wilaya kufanya kazi zao
kwa kujiamini “. Alisema Balozi Seif.
Aliwataka
na kuwaasa vijana kujiepusha na ushawishi huo wa wana siasa wa kutaka
kuwalazimisha kufanya mambo yaliyo kinyume na sheria na utaratibu wa
Nchi.
Katika
kuunga mkono ujenzi wa Tawi hilo la Mombasa Kwa mchina Mlezi huyo wa
Mkoa wa Magharibi Kichama Balozi Seif aliahidi kukamilisha ukumbi wa
Tawi hilo kwa kutoa mchango wa Jipsam, taa ,mafeni yote ukumbini hapo
pamoja na kusaidia Seti moja ya Jezi kwa Timu kati ya timu 16 zilizomo
ndani ya Tawi hilo.
Mapema akitoa Taarifa fupi ya ujenzi wa Tawi hilo Mwenyekiti wa Ujenzi ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Nd. Ahmada Yahya Abdulwakil alisema ujenzi huo ulioanza rasmi Tarehe 28 Septemba 2013 umekuja kufuatia wanachama hao kukosa ofisi ya kufanyia kazi zao za Kisiasa.
Mapema akitoa Taarifa fupi ya ujenzi wa Tawi hilo Mwenyekiti wa Ujenzi ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Nd. Ahmada Yahya Abdulwakil alisema ujenzi huo ulioanza rasmi Tarehe 28 Septemba 2013 umekuja kufuatia wanachama hao kukosa ofisi ya kufanyia kazi zao za Kisiasa.
Nd.
Ahmada alisema tawi hilo lenye ofisi zote zinazohitajika zikiwemo za
jumuiya za chama litakuwa na huduma za kisasa zinazokwenda na wakati
pamoja na ukumbi wa Mikutano ambao utakodishwa kwa shughuli za kijamii
ili kuliongezea mapato Tawi hilo.
Mwenyekiti
huyo wa Kamati ya Ujenzi wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina aliwashukuru
viongozi na wapenzi wote wa chama hicho waliojitolea kuunga nguvu
katika ujenzi wa Tawi hilo lenye hadhi ya chama chenyewe.
Katika
hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi la CCM Mombasa Kwa
Mchina Balozi Seif alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 79 wa chama cha
Mapinduzi pamoja na Jumuia zake wa Tawi hilo.
Ujenzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi Mombasa kwa Mchina hadi sasa umeshagharimu zaidi ya shilingi Milioni 45,100,000/- .
No comments:
Post a Comment