Mkufunzi wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa hana mipango ya kumuuza mshambuliaji wa kilabu hiyo Mario Baloteli wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 na ambaye amefunga mabao mawili katika mechi 15 amehusishwa na uhamisho wa Inter Milan kulingana na gazeti dello Sport.
''Hicho si kitu nilichofikiria kufanya,kusema ukweli'', alisema Rodgers.
''Tumekuwa na mechi nyingi msimu huu na kwa sasa kitu muhimu ni kukiweka kikosi hiki pamoja'',.
Liverpool ilikuwa ya pili katika jedwali la ligi ya Uingereza na walijulikana kwa mchezo wao wa kasi na 'gusa' ni 'guse'.
No comments:
Post a Comment