Aliyekuwa raia wa Marekani George Bush atasalia hospitalini wikendi hii lakini huenda akatoka hivi karibuni.
Bwana Bush mwenye umri wa miaka 90 alilazwa hospitalini siku ya jumanne baada ya kukabiliwa na tatizo la kupumua.
Msemaji wake Jim McGrath amesma kuwa hali yake imeimarika na madaktari wanajadiliana kuhusu siku ya kumtoa hospitalini.
Bush ambaye aliwahi kuwa rais wa Marekani kutoka mwaka 1989 hadi 1993 alitembelewa na familia yake siku ya krisimasi.
Miaka miwili iliopita bwana Bush alitibiwa katika hospitali hiyo hiyo kwa zaidi ya miezi miwili ambapo alikuwa anauguwa kikohozi.
No comments:
Post a Comment