TANGAZO


Tuesday, November 11, 2014

Waziri Nagu akitembelea Kiwanda cha kutengeneza Unga cha Basic Element Ltd Dar es Salaam


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu, akipatiwa maelezo kuhusu usagaji wa nafaka hadi kuaptikana kwa bidhaa ya unga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu, akipatia maelezo na mmoja wa viongozi wa Kiwanda cha kutengeneza unga cha Basic Element ltd jana Novemba 10, 2014.



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu ametembelea Kiwanda cha kutengeneza unga cha Basic Element ltd jana Novemba 10, 2014 Dar es Salaam. Waziri Nagu alitembelea sehemu za kiwanda hicho ili kuona teknolojia wanayotumia kiwandani hapo, nafaka zilizopo na namna wanavyoweka unga tayari kuuza. 
Katika zoezi hilo aliwapongeza na kuwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kwa kununua unga unaotengenezwa na kuwahakikishia wakulima kutasaidia kupata soko la kuuza mazao yao.

Mhe. Nangu alitoa wito kwa watanzania kuunga mkono kazi zinazofanyika nchini kwa kununua unga unaopatikana ikiwa ni salama na wenye ubora unaofaa kwa mlaji. 

Pamoja na hilo Waziri Nagu alisema, uwepo wa kiwanda hicho ni sehemu ya vijana kujipatia ajira kwani wanatoa nafasi 50 za ajira.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
Kitengo cha Mawasiliano
Tarehe 11 Novemba, 2014


No comments:

Post a Comment