Meneja Mauzo wa Kampuni ya Star Times Tanzania, David Kisaka akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akiwaonesha dishi na king'amuzi kipya katika uzinduzi uliofanyika kwenye duka lao, lililopo makutano ya Mitaa ya Samora na Morogoro, Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Liao Ianfang. (Picha zote na Mpigapicha Wetu)
HII ni kufuatia uzinduzi wa huduma ya DTH ambayo
humfikia mteja mahala popote bila ya kuzingatia umbali ama kama matangazo ya
digitali yamekwishazinduliwa katika eneo alipo.
Dar es Salaam,
Novemba 5, 2014 … Kile kilio cha
muda mrefu cha wakazi wa vijijini kukosa huduma za StarTimes kutokana na maeneo
yao kutokuunganishwa au kupata mawimbi hafifu sasa kimepatiwa ufumbuzi kutokana
na ujio wa huduma ya DTH.
DTH (direct-to-home) ni dishi atakalofungiwa mteja
ikiwa ni mbadala wa matumizi ya antenna za ndani ama nje. Pia huduma hii ni
mkombozi mkubwa kwa wananchi waliopo vijijini ambao aidha maeneo yao bado
matangazo ya digitali hayajazinduliwa au wanapata mawimbi hafifu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Kaimu Afisa
mtendaji Mkuu wa kampuni ya Star Media Tanzania ambao ni wasambazaji na wauzaji
wa ving’amuzi vya StarTimes nchini, Lanfang Liao amebainisha kuwa kuzinduliwa
kwa DTH ni mikakati endelevu ya
kuboresha huduma zetu na kuwafikia watanzania nchi nzima.
“StarTimes imeleta huduma hii baada ya kupokea
maoni mbalimbali kutoka kwa wateja wetu waliopo vijijini ambao wanapenda
tuwafikie.
Mbali na kuwafikia wananchi waliopo mbali pia DTH ina chaneli zaidi ya 110 za malipo nafuu na zenye muonekano wa
picha zenye ubora wa hali ya juu ambapo zipo nane za nyumbani na kwa
kuwathamini wateja wetu kati ya hizo nane mteja atalipia tatu tu huku tano
zikiwa ni bure kabisa.” Alisema Liao na kumalizia.
Naye kwa upande wake Meneja wa Mauzo wa kampuni
hiyo amesema kuwa madishi ya DTH yatakuwa yakiuzwa katika ofisi zetu na maduka
ya mawakala wetu na zitakuwa zikipatikana kwa bei ya jumla kwa kiasi cha Sh.
139,000/- kwa malipo ya mwezi pamoja na ufungaji na kwa mawakala zitapatikana
kwa Sh. 119,000/- bila ya ufungaji.
“Mteja atafungiwa dishi lake ndani ya masaa 24
baada ya kulipia na pia kutakuwa na ofa ya kipekee ya siku 15 au nusu mwezi za
bure baada ya kulipia kifurushi chochote ukipendacho kwa muda wa siku 45 yaani
mwezi mmoja na nusu.” Alisema Bw Kisaka.
“DTH imekuja kipindi mahususi kuelekea
msimu wa sikukuu na tusingependa kipindi hiki cha mapumziko kinapokuja watu
wasiweze kufikiwa na huduma zetu.
DTH
ni jibu na ufumbuzi kwa wateja wetu wote waliopo mbali na matangazo ya digitali,
hivyo basi nawasihi wawasiliane nasi ili waweze kuunganishwa na kampuni bora
kabisa ya matangazo ya digitali nchini,” aliendelea.
Bw Kisaka aliongezea kwa kusema, “Mbali na
uzinduzi wa huduma ya DTH kwa
watanzania, StarTimes pia inawaletea chaneli mpya kabisa ya Q YOU ambayo inajumuisha video fupi
fupi bora za you tube zenye maudhui ya kufurahisha,
kuchangamsha na kukuacha mwenye furaha na tabasamu usoni pindi uitazamapo.
Q YOU imekuja kuleta mabadiliko
makubwa ya vipindi tunavyovitazama katika ruinga zetu ambavyo maudhui ya
kuchekesha na kufurahisha huwa katika muda, siku na vipindi maalumu ndipo
mtazamajia anapata fursa ya kuviona.”
“Wazo la kuja na Q
YOU ni baada ya kuona kwamba kuna hitaji la kuwa na kipindi maalumu ambacho
mtu akikitazama anaondokewa na uchovu au kusahau magumu yote aliyokutana nayo
katika shughuli za siku nzima na kumfanya awe mchangamfu na mwenye nguvu
tena.
Kwa mfano unaweza ukawa umerudi kutoka kazini umechoka na kazi za huko
lakini kwa kutazama chaneli hii ukasahau yote na kujisikia mwenye nguvu tena za
kufanya mambo mengine.”
Meneja huyo wa mauzo
alimalizia kwa kuwasihi wateja na
watanzania kwa ujumla wajiunge na kulipia vifurushi vya UHURU na KILI
vinavyopatikana kwa Tsh. 20,000 na 30,000 pekee kwa watumiaji wa antenna
na kwa wale wateja wetu wa dishi wanaweza kufurahia huduma hii kwa kulipia
kifurushi cha Smart kwa Sh. 32,000/- tu.Hivyo ningewaomba wateja wetu
watembelee maduka yetu na waunganishwe na huduma zetu na kufurahia chaneli nyinginezo.
|
No comments:
Post a Comment