TANGAZO


Thursday, November 6, 2014

Rais awaapisha Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Katibu Tawala na Mabalozi



Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Dk. Yohana Budeba, Ikulu Dar es Salaam leo, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi vitendea kazi, Mhandisi Mbogo Futakamba, baada ya kumwapisha, Ikulu Dar es Salaam leo, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Dk. Donan Mmbando, Ikulu Dar es Salaam leo, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.




Walioapishwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu na Katibu Tawala, wakipiga picha pamoja na Rais Kikwete.


Rais Jakaya Kikweta, akipiga picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Donan Mmbando pamoja na familia yake, mara baada ya kumwapisha.





Dk. Mbando akizungumza na waandishi wa habara mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.


Dk. Ibrahim Hamis Msengi akila kiapo cha utii kwa Rais Jakaya Kikwete, wakati alipoapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Bi. Amina Juma Masenza, akila kiapo cha utii kwa Rais, wakati alipokuwa akiapa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Bi. Halima Omar Dendego, akiapa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mbele ya Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera, John Mongella (kulia), Ikulu Dar es Salaam leo, wakati alipowaapisha wakuu wa mikoa, makatibu wakuu, makatibu tawala wa mikoa na balozi mpya, aliowateua hivi karibuni. Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha kabla ya uteuzi huo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi vitendea kazi Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera, John Mongella, mara baada ya kumwapisha Ikulu Dar es Salaam leo.
Bw. Shelukindo, akipokea vitendea kazi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kumwapisha kuwa Balozi, Ikulu Dar es Salaam leo.
Wakuu wapya wa Mikoa wakipiga picha ya kumbukumbu na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwaapisha Ikulu Dar es Salaam leo.

Bi. Amina Masenza akipiga picha ya kumbukumbu na familia yake pamoja na Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kumwapisha Ikulu jijini leo.
Bi. Halima Omar Dendego, akipiga picha ya kumbukumbu na familia yake pamoja na Rais Kikwete, mara baada ya kumwapisha Ikulu jijini leo.
Bw. John Mongella na Familia yake, wakipiga picha ya kumbukumbu na Rais Kikwete, mara baada ya kula kiapo Ikulu leo.
Bw. Shelukindo, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Rais Kikwete, mara baada ya kuapishwa na Rais Kikwete jijini leo.

Wakuu wapya wa Mikoa wakipiga picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kula kiapo Ikulu jijini leo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa kwenye Mawasiliano, mara baada ya kuaapisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala na Mabalozi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wazazi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella, Mama Mongella (kulia) na Baba Silvin Mongella (kushoto), wakati wa hafla hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kula kiapo, katika hafla hiyo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Hni alima Omar Dendego, akiwa katika picha ya pamoja na familia yake wakati wa hafla hiyo, Ikulu jijini leo.

Na Anitha Jonas, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Profesa Jakaya Mrisho Kikwete  leo  amewaapisha viongozi  kumi na moja aliyowateua, ambao ni  Makatibu  Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Mikoa,Mabalozi na Makatibu Tawala za Mikoa mbalimbali.
Viongozi hao, waliapishwa leo jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi  Ombeni Sefue.

Miongoni  wa  viongozi  walioapishwa  ni   aliyekuwa  Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye  ameteuliwa kuwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando, ambapo  amesema katika swala la upungufu wa  dawa  mahospitalini atajitahidi katika bajeti ijayo kujenga hoja na kutetea  manunuzi ya dawa.
 “Serikali ina   mpango mbadala wa utoaji wa vifaa vya afya kwani imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya afya ikiwemo kuangalia  kuwepo na usawa wa gharama za huduma afya  nchini,” alisema.

Naye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba  ameapishwa kuwa  Katibu wa wizara amesema Wizara ya Maji imefanikiwa katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa(BRN) kwa kufikia  53% kutoka 40% katika kusambaza maji safi maeneo ya vijijini.
Aliongeza kwamba Serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuboresha mitambo ya maji Ruvu chini na kujenga visima ili kuwawezesha wakazi wa jijini Dar es Salaam kupata maji ya kutosha.
Aidha aliyekuwa  Mtumishi Mwandamizi Ofisi ya Rais, Jack Mgendi Zoka ameapishwa  kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, ambapo ameahidi kwenda kuiwakilisha vyema Tanzania huko na kuisaidia nchi kupata fursa nyingi na kutafuta wahisani wa kuchangia maendeleo katika taifa.
Viongozi  wengine, waliapishwa  ni Jonny Vianney Mongela ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,  hapo  awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, ambapo  amesema anaamini ushirikiano mzuri atakaoupata kutoka kwa wananchi ndiyo utakao changia mafanikio makubwa katika mkoa huo,pia kwa kupita uzoefu wake na ataenda kusimamia  yote yaliyokwisha  kuanzishwa ili kuleta mafanikio zaidi.

Naye Bi. Amina Juma Masenza ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa , amesema ataenda kuweka msisitizo wa vipao mbele vyote vya taifa katika mkoa wake na pia amesema anaamini  kufanya kazi kwa ushirikiano ndio njia ya kuleta mafanikio makubwa katika mkoa huo.
Wengine waliaopishwa ni  Mkuu wa Mkoa Mtwara Bi. Halima Omari Dendego,  ambaye alikuwa Mkuu wa  Wilaya ya Tanga amesema changamoto kubwa katika mkoa wake ni kupandisha pato la mkazi wa Mtwara na kupitia miradi mbalimbali iliyopo mkoa huo ikiwemo gesi kupatikana kwa mafanikio, katika swala hilo  pamoja kusimamia maswala ya elimu katika mkoa huo.

Aidha naye  Samuel  Shelukindo  aliapishwa kuwa Balozi na kupewa wadhifa  wa kuwa Mshauri wa Rais masuala ya Kidiplomasia,alisema anamshukuru Rais kwa uteuzi huo na ameahidi kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa huku akingalia maslahi ya taifa kwa ujumla.
Katika hafla hiyo Makatibu Tawala walioapishwa ni Addo Mapunda na Charles Amos   Pallangyo.

No comments:

Post a Comment