TANGAZO


Sunday, November 9, 2014

Miaka 25 ya ukuta wa Berlin kuporomoshwa

Sherehe katika Brandenburg Gate, Berlin
Sherehe zinafanywa Ujerumani kuadhimisha miaka 25 tangu ukuta wa Berlin kuporomoshwa.
Ukuta huo uligawa Berlin Magharibi na Mashariki iliyokuwa ya kikokiministi.
Ulipobomolewa ulipelekea Ujerumani Mashariki na Magharibi kuungana tena, na kusaidia kumaliza Vita Baridi.
Kiongozi wa Ujerumani, Bibi Merkel, amesema kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin kulitoa ujumbe wa matumaini kwa watu wa nchi ambako haki za kibinaadamu bado zinakiukwa.
Bibi Merkel, ambaye akiishi Ujerumani Mashariki wakati huo, alisema maadhimisho hayo ni siku ya furaha, lakini piya siku ya kuwakumbuka wale waliokufa walipojaribu kukimbilia Magharibi au walifungwa na Ujerumani Mashariki.
Alihudhuria ibada kanisani kuwakumbuka wanyonge wa utawala wa Kikoministi wa Ujerumani mashariki.
Na Papa Francis aliwasifu wale waliosaidia kuporomosha ukuta huo na aliwaomba watu waendeleze umoja, ili kuvunja vizuizi vyote vinavyogawa ulimwengu.
Kati ya wageni waliojumuika na Bibi Merkel katika sherehe hizo ni kiongozi wa zamani wa chama cha wafanyakazi wa Poland, Lech Walesa, na rais wa zamani wa Umoja wa Sovieti, Mikhail Gorbachev.

No comments:

Post a Comment