TANGAZO


Monday, November 3, 2014

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), yawatupa Mahabusu Menyekiti wa Bodi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, akifafanua jambo wakati akiwahoji Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, James Andilile wakati kamati hiyo, ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake kilichofanyika leo, Ofisi za Bunge, Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filkunjombe. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPDC, James Andilile, akila kiapo, wakati kamati hiyo, ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake kilichofanyika leo jijini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda, akila kiapo, wakati kamati hiyo, ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake kilichofanyika leo jijini.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filkunjombe (kushoto) na Mwanasheria wa Bunge, Nenelwa Mwihambi (kulia), wakisikiliza majibu yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa TPDC, wakati wa kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPDC, James Andilile, akitoa maelezo ya utetezi, wakati alipotakiwa na kamati hiyo kujibu maswali mbalimbali juu ya kuinyima taarifa muhimu PAC. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPDC, James Andilile, akitoa maelezo ya utetezi, wakati alipotakiwa na kamati hiyo kujibu maswali mbalimbali juu ya kuinyima taarifa muhimu PAC. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPDC, James Andilile, akitoa maelezo kwa kamati hiyo, wakati alipokuwa akihojiwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, akiwahoji viongozi hao. Kushoto ni Makamu wake, Deo Filkunjombe.
 Kamati ya PAC, ikiwa katika kikao hicho.
 Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ikiwa katika kikao hicho. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda, akijibu na kuyatolea ufafanuzi maswali aliyokuwa akiulizwa na Kamati ya PAC. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPDC, James Andilile.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda, akijibu na kuyatolea ufafanuzi maswali aliyokuwa akiulizwa na Kamati ya PAC. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPDC, James Andilile.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (kushoto), akijibu na kuyatolea ufafanuzi maswali aliyokuwa akiulizwa na Kamati ya PAC. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (kushoto), akijibu na kuyatolea ufafanuzi maswali aliyokuwa akiulizwa na Kamati ya PAC.
Baadhi ya wajumbe wa PAC wakifuatilia jinsi viongozi hao wa TPDC, walivyokuwa wakijibu maswali ya kamati hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filkunjombe, akitaka ufafanuzi kwa viongozi hao juu ya mahesabu wanawajibika kwa nani ?
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filkunjombe, akiwauliza swali viongozi hao juu ya mahesabu yao, wanawajibika kwa nani ?
Mwanasheria wa Bunge, Nenelwa Mwihambi (kulia), akisoma kifungu cha Kanuni za Bunge kwa viongozi hao wa TPDC, wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kwenda kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, James Andilile (nyuma), wakipanda gari la Polisi baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake kilichofanyika leo, Ofisi za Bunge, Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda (aliyejificha kushoto) wakiwa kwenye gari la Polisi wakipelekwa kwenda rumande.

No comments:

Post a Comment